Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Aidha atajua kuwa upotofu na shaka imewashika wengi katika wale waliokuja nyuma kwa sababu ya kukitupilia mbali Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao, kupuuza ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuacha kuisoma njia ya wale wa awali walitoangulia na kwenda kwa watu ambao, kwa kukubali wao wenyewe, hawamtambui Allaah. Aidha ummah unashuhudia jambo hilo na ukiongezea juu yake dalili zingine nyingi. Sina lengo la kumtaja mmoja, isipokuwa nitataja sampuli zote za watu hawa.
MAELEZO
Sababu iliyowafanya wale waliokuja nyuma kuingia ndani ya upotofu ni kuitupilia mbali Qur-aan. Hawaitumii kama hoja. Badala yake wanajenga hoja kwa mantiki, falsafa na istilaha nyenginezo kama vile kiwiliwili, dutu, isiyo ya mwili na mpandiano. Haya ndio mambo yao. Ama yule ambaye ameichukua ´Aqiydah yake kutoka ndani ya Qur-aan, Sunnah na ´Aqiydah ya Salaf ndiye anayepita juu ya njia ilionyooka.
Ibn Taymiyyah lengo lake haikuwa mtu mmoja, bali mkusanyiko wao. Namna hii anatakiwa kuwa mwanafunzi wakati anapomraddi mpinzani; asitaje majina yao bali anatakiwa kutaja ´Aqiydah na makosa yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akitaja majina pindi anapokosoa, bali akisema:
”Inakuweje baadhi ya watu… ”[1]
Hii ndio ilikuwa njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akitaja kosa na si mtu mwenye kosa hilo. Isipokuwa mtu huyo kama ni mpotofu na watu wamedanganyika na kuhadaika naye; katika hali hii ni lazima atajwe kwa jina ili watu wamtambue. Wanazuoni wa Hadiyth huwataja watu kwa majina na kulenga unyonge wa kumbukumbu zao, mwongo, muundaji na mzushi ili watu wasighurike naye. Kwa maana nyingine hali na dharurah ikipelekea kumlenga mtu kwa jina mtu anafanya hivo. Vinginevyo bora mtu asifanye hivo.
[1] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 105-106
- Imechapishwa: 18/08/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket