66. Sura ya saba: Kudai haki ya kuweka Shari´ah, kuhalalisha na kuharamisha

Uwekaji wa hukumu ambazo waja wanatembelea juu yake katika ´ibaadah zao, miamala yao na mambo yao mengine yote uwekaji ambao unatatua mizozo baina yao na kuyamaliza magomvi ni haki ya Allaah (Ta´ala) ambaye ndiye Mola wa watu na Muumbaji wa viumbe:

أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Tanabahi! Uumbaji ni Wake pekee na kupitisha amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

Yeye ndiye anajua zaidi yanayoendana na waja Wake na hivyo akawawekea nayo. Anawawekea Shari´ah kwa hukumu ya uola Wake na anazikubali hukumu zao kwa hukumu ya uungu Wake. Pamoja na hivyo manufaa katika hayo bado ni yenye kurudi kwao. Amesema (Ta´ala):

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[2]

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ

”Jambo lolote lile mlilokhitilafiana kwalo, basi hukumu yake ni kwa Allaah. Huyo ndiye Allaah, Mola wangu, Kwake nategemea na Kwake narejea kutubia.”[3]

Amewakemea (Subhaanah) waja kujifanyia waweka Shari´ah wengine mbali na Yeye pale aliposema:

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

“Je, wanao washirika waliowawekea Shari´ah katika dini yale ambayo Allaah hakuyatolea idhini?”[4]

Anayekubali Shari´ah isiyokuwa ya Allaah basi amemshirikisha Allaah (Ta´ala). Zile ´ibaadah ambazo hazikuwekwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Bid´ah. Kila Bid´ah ni upotevu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”[5]

 Katika upokezi mwingine:

“Mwenye kufanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[6]

Yale ambayo hayakuwekwa na Allaah wala Mtume Wake katika siasa na hukumu baina ya watu basi hiyo ni hukumu ya Twaaghuut na hukumu ya kipindi cha kikafiri:

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.”[7]

Vivyo hivyo kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Allaah (Ta´ala). Haijuzu kwa yeyote kushirikiana Naye katika jambo hilo. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ

“Wala msile katika ambavyo havikutajiwa jina la Allaah, kwani hakika huo ni ufaska, na hakika mashaytwaan wanawanong´oneza wapenzi wao wabishane nanyi – na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.”[8]

Amefanya (Subhaanah) kule kuwatii mashaytwaan na wapenzi wao katika kuhalalisha aliyoharamisha Allaah ni kumshirikisha Yeye (Subhaanah). Kadhalika yule mwenye kuwatii wanachuoni na viongozi katika kuharamisha yale aliyohalalisha Allaah au kuhalalisha yale aliyoharamisha Allaah basi amewafanya kuwa waungu badala ya Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ

“Wamewafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni waungu badala ya Allaah na al-Masiyh mwana wa Maryam na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Mungu mmoja. Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye – utakasifu ni Wake kutokamana na yale yote wanayomshirkisha.”[9]

Imepokelewa katika Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsomea Aayah hii ´Adiyy bin Haatim at-Twaa-iy (Radhiya Allaahu ´anh) ambapo akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hatukuwa tukiwaabudu.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, si walikuwa wakihalalisha yale yaliyoharamishwa na Allaah nanyi mnayahalalisha na wakiharamisha yale yaliyoharamishwa na Allaah nanyi mnayaharamisha?” Akajibu: “Ndio.” Akasema: “Huku ndio kuwaabudu.”[10]

Ikawa kuwatii kwao katika kuhalalisha na kuharamisha badala ya Allaah ni kuwaabudu na shirki. Nayo ni shirki kubwa inayopingana na Tawhiyd ambayo ndio inayofahamishwa na “Laa ilaaha illa Allaah”[11]. Miongoni mwa yanayofahamishwa nayo ni kwamba kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Allaah (Ta´ala). Hali ikiwa namna hii kwa yule anayewatii wanachuoni na wachaji katika kuhalalisha na kuharamisha mambo yanayokwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah – na wakati huohuo anajua mukhalafa huo – pamoja na kwamba wao wako karibu zaidi na elimu na dini. Pengine hata kosa lao linatokamana na Ijtihaad ambayo hawakupatia haki ndani yake ingawa ni wenye kupewa ujira kwa jambo hilo. Tusemeje juu ya wale ambao wanazitii kanuni ambazo zimetungwa na makafiri na wakanamungu na akazileta kwenye miji ya waislamu na akahukumu kwazo baina yao? Hakika huyu amewafanya makafiri kuwa ni waungu badala ya Allaah ambao wanamtungia hukumu mbalimbali, wanamhalalishia ya haramu na wanahukumu kati ya watu.

[1] 07:54

[2] 04:59

[3] 42:10

[4] 42:21

[5] al-Bukhaariy (2550) na Muslim (1718).

[6] Muslim (4468).

[7] 05:50

[8] 06:121

[9] 09:31

[10] at-Tirmidhiy amepokea mfano wake (3104).

[11] Fath-ul-Majiyd, uk. 107.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 126-128
  • Imechapishwa: 31/03/2020