Ngazi ya pili ya wafungaji ni wale wanaofunga duniani kwa ajili ya Allaah pekee ambapo wakahifadhi vichwa na matumbo yao na wakakumbuka kifo na wanakusudia Aakhirah ambapo wakaacha dunia na mapambo yake. Huyu sikukuu ya kula kwake itakuwa siku ile atapokutana na Mola Wake na atafurahi kwa kule kumuona.

Yule ambaye kutokana na amri ya Allaah amefunga ambapo akajizuia na vile anavyotamani basi atavikuta hiyo kesho Peponi. Na yule ambaye atafunga kwa ajili ya Allaah basi sikukuu yake itakuwa siku ya kukutana Naye:

مَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ اللَّـهِ فَإِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ لَآتٍ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

“Anayetaraji kukutana na Allaah, basi hakika muda uliopangwa na Allaah utafika pasi na shaka. Naye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa kila kitu.”[1]

Enyi wenye kutubia! Fungeni ijapo siku moja kutokamana na matamanio ya hawaa ili muweze kupata sikukuu ya kula siku ya mkutano.

[1] 29:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 81
  • Imechapishwa: 01/05/2021