47. Maimamu waajiriwa wanaosafiri Ramadhaan na kuacha misikiti yao

Swali 47: Ni upi mwongozo wako juu ya baadhi ya maimamu wa misikiti ambao wanaacha misikiti yao katika Ramadhaan na wanaenda Makkah kufanya ´Umrah na kuswali katika msikiti Mtakatifu katika kipindi cha mwezi huu?

Jibu: Maelekezo yetu kwa watu hawa ni kwamba wanatakiwa kutambua kuwa kubaki katika misikiti yao ili watu wakusanyike kwayo na kutekeleza wajibu wao ambao wamejikubalisha mbele ya serikali yao ni bora kuliko kwenda kukaa na kuswali Makkah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutaja kuhusu kitendo cha kwenda Makkah katika Ramadhaan isipokuwa tu kufanya ´Umrah peke yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“´Umrah katika Ramadhaan inalingana na kufanya hajj.”

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakutaja jambo la kukaa huko. Hata hivyo hapana shaka kwamba kukaa Makkah ni bora kuliko kukaa mahali kwengine. Lakini hili linamuhusu yule ambaye hana kazi aliofungamana nayo mbele ya serikali yake na ambayo analazimika kuitimiza.

Nasaha zangu kwa watu hawa ni kwamba wakitaka kufanya ´Umrah waende na kurejea pasi na kuchelewa. Hivyo watakuwa wametekeleza yale yanayowawajibikia juu ya ndugu na watawala wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 40
  • Imechapishwa: 02/05/2021