66. Je, kuwatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah kwa majina ni usengenyi ulioharamishwa?

Swali 66: Pindi baadhi ya wanafunzi wanapowasikia wanafunzi wengine au wanazuoni wanatahadharisha Bid´ah na Ahl-ul-Bid´ah na mifumo yao, wanataja uhakika wa yale waliyomo na wakawaraddi (wakati mwingine huenda wakataja majina ya baadhi yao, ingawa wameshakufa, ili watu wasifitinishwe nao) kwa lengo la kuitetea dini hii na kufichukua ubabaishaji wa wenye kubabaisha wanaougawanya ummah na kusababisha mipasuko, wanasema eti kufanya hivo ni usengenyi ulioharamishwa. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Ikiwa kosa au upindaji umetambuliwa na kuna umuhimu kuwataja kwa majina wale wahalifu ili watu wasidanganyike nao, na khaswa wale watu walio na upindaji katika fikira au wako na upindaji katika mfumo na watu hao wanatambulika kati ya watu na wanawajengea dhana nzuri, basi hapana neno kuwataja kwa majina yao na kutahadharisha dhidi ya mifumo yao. Wakati wanazuoni wanapowakosoa na kuwasifu wale wasimuliaji wanawataja kwa majina wao na zile sifa wanazikosoa. Si kwa ajili ya shaksia zao, bali kwa ajili ya kutakia kheri ummah wasichukue vitu vinavoidhuru dini au kumsemea uwongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kwa hivyo kanuni mtu kwanza anatakiwa kuzindua kosa na asimtaje mtu kwa jina ikiwa hilo linapelekea katika madhara au katika kumtaja hakuna faida. Lakini ikiwa kuna umuhimu kumtaja kwa jina ili watu wajihadhari kutokana na mfumo wake, basi kufanya hivo ni katika kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wao wa kawaida. Hilo khaswa pale anapokuwa na uchangamfu kati ya watu na wanamdhania vizuri na kanda na vitabu vyake. Katika hali hiyo ni lazima kumbainisha na kuwatahadharisha watu kutokana naye. Kwa sababu kunyamaza kunawadhuru watu. Ni lazima kumfichukua, sio kwa ajili ya kumjeruhi au kumkashifu, bali ni kwa ajili ya kumtakia mema Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, viongozi wa waislamu na watu wao wa kawaida.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 172-173
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy