66. Hakuna kitu kigumu kabisa kama kuwa na subira

Katika mlango huu subira inagawanyika sehemu mbili: mahitaji ya kitendo hicho na urahisi wake. Mambo yote hayo mawili yakikutana basi subira inakuwa ngumu. Mambo yote hayo mawili yakipotea inakuwa ni rahisi kusubiri. Kimoja katika hayo kikipatikana na kingine kikakosekana inakuwa ni rahisi kusubiri kwa mtazamo mmoja na vigumu kwa mtazamo mwingine.

Mwenye kuhitaji kuua, kuiba, kunywa pombe, kuvuta bangi na machafu mengine na wakati huo huo hayo yaliyotajwa yakawa si rahisi basi kusubiri kwake itakuwa ni rahisi sana.

Mwenye kuhitaji hayo yaliyotajwa na yakamuwia sahali basi kusubiri kwake itakuwa ni vigumu sana.

Ndio maana mtawala anayesubiri juu ya dhuluma, kijana anayesubiri juu ya machafu na tajiri anayesubiri juu ya mambo ya ladha na matamanio wana ngazi za juu mbele ya Allaah. Hakuna anayewafikia isipokuwa yule atayekuwa na subira kama walionayo.

Hali kadhalika yule mwenye kusubiri kwa kufa mtoto wake, wazazi wake, jamaa zake na marafiki zake. Pamoja na hivyo yule aliyefikwa na msiba akawa na subira na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah. Aidha akaikumbusha familia yake kusubiri kwa msiba na akawakataza kurarua nguo, kujipiga mashavu na kuzungumza maneno yasiyofaa. Huyu ana thawabu nyingi na ujira mkubwa usiojua yeyote isipokuwa Allaah.

Mja anapoonja utamu wa maasi kisha akatubia na kuwa mvumilivu kutotumbukia ndani yake, basi tawbah yake inazingatiwa kuwa ni ya kweli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 148
  • Imechapishwa: 05/11/2016