66. Bwana ambaye ´Arshi ilitikisika kwa ajili yake

63 – Jaabir amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema wakati ambapo jeneza la Sa´d bin Mu´aadh likiwa mbele yao kwa ajili ya kuliswalia:

”´Arshi ya Mwingi wa rehema imetikisika kwa ajili yake.”

Tamko ni la Muslim[1]. Imekuja kupitia njia nyingine kwamba Jaabir amesema:

”Jibriyl alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Ni nani mja huyu mwema aliyekufa? Milango ya mbingu imefunguliwa kwa ajili yake na ´Arshi imetikisika kwa ajili yake.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatoka nje na akaona kuwa ni Sa´d. Akaketi karibu na kaburi lake… ”

Ameipokea an-Nasaa´iy.

[1] al-Bukhaariy pia ameipokea. Nimeitaja katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (562). Ule upokezi mwingine umepokelewa pia na Ahmad (03/327). Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Abu Ja´far bin Abiy Shaybah ameipokea katika ”al-´Arsh” (01/133 – muswada).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 108-109
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy