62 – Abu Sa´iyd ameeleza:
”Myahudi mmoja alimtaja Muusa kwa namna ya kwamba ni kana kwamba alimfadhilisha mbele ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambapo yule Mnusuraji akampiga kofi. Myahudi yule akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumshtaki bwana yule, ambapo akasema: ”Msinifadhilishe mbele ya Mitume wengine. Mimi ndiye wa kwanza ambaye ardhi itamfufua. Tahamaki itakuwa ni Muusa ambaye ameishika moja ya nguzo za ´Arshi. Sijui kama yeye ndiye aliyefufuliwa wakati wa kuzimia mara ya kwanza au ni baada yangu.”
Muslim ameipokea kutoka kwake:
”Msifadhilishe kati ya Mitume.”[1]
[1] Uhakika wa mambo ni kwamba Muslim amepokea mfano wake kwa ukamilifu, lakini katika tamko lake amerejesha vilevile katika Hadiyth ya Abu Hurayrah iliotangulia. al-Bukhaariy pia ameipokea kwa ukamilifu wake katika maeneo mawili. Vivyo hivyo ndivo alivofanya Ahmad Ahmad (3/33) na Abu Daawuud (468) kwa ufupisho, na ipo vilevile kwa Ahmad (3/31).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 108
- Imechapishwa: 26/06/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
62 – Abu Sa´iyd ameeleza:
”Myahudi mmoja alimtaja Muusa kwa namna ya kwamba ni kana kwamba alimfadhilisha mbele ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambapo yule Mnusuraji akampiga kofi. Myahudi yule akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumshtaki bwana yule, ambapo akasema: ”Msinifadhilishe mbele ya Mitume wengine. Mimi ndiye wa kwanza ambaye ardhi itamfufua. Tahamaki itakuwa ni Muusa ambaye ameishika moja ya nguzo za ´Arshi. Sijui kama yeye ndiye aliyefufuliwa wakati wa kuzimia mara ya kwanza au ni baada yangu.”
Muslim ameipokea kutoka kwake:
”Msifadhilishe kati ya Mitume.”[1]
[1] Uhakika wa mambo ni kwamba Muslim amepokea mfano wake kwa ukamilifu, lakini katika tamko lake amerejesha vilevile katika Hadiyth ya Abu Hurayrah iliotangulia. al-Bukhaariy pia ameipokea kwa ukamilifu wake katika maeneo mawili. Vivyo hivyo ndivo alivofanya Ahmad Ahmad (3/33) na Abu Daawuud (468) kwa ufupisho, na ipo vilevile kwa Ahmad (3/31).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 108
Imechapishwa: 26/06/2024
Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
https://firqatunnajia.com/65-mtu-wa-kwanza-atakayefufuka-siku-ya-qiyaamah/