65. Kuwa na subira juu ya mali, wake na watoto

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewatahadharisha waja Wake waumini juu ya fitina ya mali, wake na watoto. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

“Enyi mlioamini! Yasikushughulisheni mali zenu na wala watoto wenu na ukumbusho wa Allaah; na atakayefanya hivyo basi hao ndio waliokhasirika.” 63:09

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ

”Hakika mali zenu na watoto wenu si jengine isipokuwa anakujaribuni; na kwa Allaah kuna ujira mkubwa.” 64:15

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ

”Enyi mlioamini! Hakika kunaweza kuwepo maadui wenu katika wake zenu na watoto wenu; basi tahadharini nao!” 64:14

Watu wengi wanazifahamu kimakosa Aayah hizi wanapofikiri kuwa uadui uliyotajwa unahusiana na chuki na mabishano. Mambo sivyo. Bali inahusu uadui wa mapenzi yanayowazuia mababa kutokamana na Hijrah, Jihaad, kufunza elimu na matendo mema mengine. Hii ndio maana ya yale yaliyosemwa na Ibn-ul-Qayyim.

Kinacholengwa ni kwamba yule mwenye kusubiri katika kipindi chepesi amejikinga kutokamana na fitina za mali. Huyu anaweza kutenda dhambi na kutumia vibaya pesa. Kwa ajili hiyo ndio maana akawa na thawabu chungunzima na fadhila kubwa. Hali kadhalika yule mwenye kusubiri juu ya kuwalea watoto na maudhi ya wake. Huyu ana daraja za juu. Sio wake na watoto wote ni maadui kwa mababa. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema wakati wa maneno ya Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ

”Enyi mlioamini! Hakika kunaweza kuwepo maadui wenu katika wake zenu na watoto wenu; basi tahadharini nao!” 64:14

“Bi maana baadhi ya wake na watoto na si wote.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 144-146
  • Imechapishwa: 03/11/2016