64. Namna hii ndivo anataamiliwa anayekwenda kinyume na mfumo wa Salaf?

Swali 64: Kuna watu waliotuzunguka wanaoenda kinyume na misingi ya Salafiyyah na wakainusuru mifumo mingine. Wanawasifu waanzilishi wake na wenye kuifikiria. Je, ni lazima kuwataja kwa majina ili watu wajihadhari nao na wasidanganyike nao na mifumo yao?

Jibu: Anayesifu mfumo wa Salaf na akasifu mifumo inayopingana na mfumo wa Salaf na akawasifu wafuasi wake anazingatiwa ni katika wahalifu. Ni lazima kumlingania na kumshauri. Ima arejee katika haki au asuswe na akatwe.

Sidhani kuwa watu kama hao wako katika nchi hii ambayo imejengeka juu ya Tawhiyd na mfumo wa Salaf. Lakini kunaweza kuwepo watu wanaowadhania vyema watu wenye mirengo inayokwenda kinyume na wakawa hawajui uhakika wa yale waliyomo. Wakibainishiwa haki kwa njia nzuri basi wakiakubali – kwa idhini ya Allaah.

Aidha nawanasihi watu kutofanya haraka ya kuwahukumu watu, kuwatuhumu kwenda kinyume na kuwakimbiza mbali[1].

[1] Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Yule ambaye anawajengea dhana nzuri na akadai kuwa haijui hali yao, atatambulishwa hali yao. Ikiwa baada ya hapo ataendelea kuwa pamoja nao na akaacha kuwakaripia, ataunganishwa pamoja nao.

Kuhusu ambaye atasema kuwa tafsiri yao ina mtazamo fulani unaoafikiana na Shari´ah, basi huyo ni katika wakuu na viongozi wao. Kama yuko na akili, basi atatambua uwongo wake katika aliyoyasema.” (Majmuu´-ul-Fataawaa (2/133))

Shaykh Bakr Abu Zayd amesema:

”Kila ambaye atamnusuru mzushi, akamtukuza au akavitukuza vitabu vyake, akavieneza kati ya waislamu, akamtukuza yeye na vyenyewe, akaeneza zile Bid´ah na upotofu uliyomo ndani yake na asiwafichukue ile ´Aqiydah iliyopinda walionayo, ni mzembe katika jambo lake. Ni lazima kuikata shari ya mtu huyo ili isisambae kwa waislamu wengine.” (Hajr-ul-Mubtadiy´, uk. 48)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 171
  • Imechapishwa: 30/06/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy