al-´Ayyaashiy amesema:
“al-Husayn bin Khaalid ameeleza kuwa Abul-Hasan amesema: “Ni vipi unaisoma Aayah hii:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ
“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa nyinyi ni waislamu.”[1]
Kitu gani?” Nikasema: “Nanyi ni waislamu.” Akasema: “Ametakasika Allaah! Unatarajia watakuwa na imani na kuwaita “waumini” ilihali Yeye amewaamrisha kuwa waislamu. Imani iko juu kuliko Uislamu.” Nikasema: “Hivyo ndivyo ilivyosomwa kwa mujibu wa Zayd.” Akasema: “Isomwe kwa mujibu wa kisomo cha ´Aliy. Ndio kisomo ambacho Jibriyl aliteremka nacho kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nacho ni:
وَلاَ تَمُوتُنَّ إِلاَّ وَأَنتُم مُّسْلِمُون لرسول الله ثم الامام من بعده
“… na wala msife isipokuwa nyinyi ni wenye kujisalimisha kwa Mtume wa Allaah halafu kwa imamu baada yake.”[2]
Allaah amemtakasa Abul-Hasan kutokamana na uongo huu mkubwa kwa Allaah, Kitabu Chake na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah amewatakasa vilevile Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuongeza au kupunguza herufi kutoka humo. Katika maneno haya wanatuhumiwa Maswahabah ya kwamba wameondosha yale ambayo yamezuliwa na waongo. Nyongeza hiyo imezidishwa na Baatwiniyyah ili kumzulia uongo Allaah na kuwatukana Maswahabah na Ummah.
Na wala Allaah hakumuamrisha yeyote kujisalimisha kwa Mtume kisha imamu baada yake. Uislamu katika Qur-aan haukukusudiwa jengine isipokuwa kutekelezewa Allaah. Ujisalimishaji huu ni ule unyenyekevu kwa ukubwa wa Allaah ambao ni kumtekelezea Allaah peke yake. Allaah (Ta´ala) amesema pindi alipokuwa akimsifu Ibraahiym:
إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ
“Pindi Mola wake alipomwambia: “Jisalimishe!” Akasema: “Nimejisalimisha kwa Mola, wa walimwengu.”[3]
[1] 03:102
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/193).
[3] 02:131
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 102
- Imechapishwa: 03/04/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 102
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/64-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-nane-wa-aal-imraan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)