63. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa saba wa Aal ´Imraan

al-´Ayyaashiy amesema:

“Yuunus bin Dhwibyaan amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema: “Imeteremshwa namna hii:

لَن تَنَالُواْ الْبِرَّ حَتَّى تُنفِقُواْ ما تُحِبُّونَ

“Hamtoweza kuufikia wema mpaka mtoe vile mnavyovipenda na hakuna chochote mnachokitoa isipokuwa hakika Allaah kwacho ni mjuzi.”[1]

Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokamana na upotoshaji na ukafiri huu. Hivi kweli Abu ´Abdillaah alikuwa mroho na mwenye tamaa mpaka atake kupora mali za watu? Kamwe!

Binaadamu ameumbwa kwa maumbile ya kuipenda nafsi na mali yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا

“Na mnapenda mali upendo mkubwa wa kupita kiasi””[2]

وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ

“… na hakika yeye nii mwingi mno wa kupenda [kukusanya] mali.”[3]

Je, Allaah amewaamrisha watu wote, au waumini, kuitoa mali yao yote katika njia ya Allaah, sembuse kuitoa kuwapa baadhi ya watu? Hakika upotoshaji huu wenye kushtua unaofanywa na Baatwiniy huyu na mfano wake haufanywi kwa ajili ya familia ya Mtume isipokuwa ni kwa ajili ya matumbo yao yaliyojaa mali ya haramu.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/184).

[2] 89:20

[3] 100:08

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 03/04/2017