63. Vipi wanaweza kuwa wajuzi zaidi kuliko warithi wa Mitume?

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Ni vipi basi vizazi vya wanafalsafa, vifaranga vya wahindi na wagiriki, waabudia moto, washirikina, wapotofu wa kiyahudi, manaswara, wasabai na mfano wao kuwa wajuzi zaidi kuliko warithi wa Mitume na wale watu wa Qur-aan na waumini?

MAELEZO

Ni wale wanafunzi wa wanafalsafa wanaojidai kuwa na hekima na utambuzi pasi na kurejea katika Wahy na kuwafuata Mitume. Wao wanadai kuwa ni bora na wajuzi zaidi kuwashinda Mitume. Wengi wao walikuwa wanaishi katika Ugiriki ya zamani. Walijifunza kutoka kwao, wakarithi ujinga na fikira zao mbaya na zilizopinda na wakawapa mgongo Mitume. Kulikuwepo wanafalsafa katika wagiriki na wahindi. Waabudia moto ni wale wenye kuabudu moto. Washirikina ni wale wenye kuabudia masanamu. Hawana kitabu na hawaamini kitabu wala Mtume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 102
  • Imechapishwa: 13/08/2024