3 – Shaykh na ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Imaam Maalik na wengineo katika Salaf waliulizwa kuhusiana na maneno Yake (Ta’ala):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]
Amelingana juu vipi?” Akajibu: “Kulingana juu kunatambulika na namna haitambuliki, ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah.” Akabainisha kuwa Kulingana juu kunajulikana na kwamba namna yake haitambuliki. Hayohayo ndio yanatakiwa kusemwa juu ya yale yote ambayo Allaah amejisifu Mwenyewe.”[2]
4 – Shaykh na ´Allaamah Muhammad al-Amiyn ash-Shanqwiytwiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Unapaswa kutambua ya kwamba watu wengi wanasema kwamba Aayah zinazohusiana na sifa haziko wazi. Hili ni kosa kwa upande mmoja na inawezekana kwa upande mwingine, kama alivyobainisha Imaam Maalik bin Anas. Maana zinajulikana kwa waarabu. Imaam Maalik amesema:
”Kulingana juu kunatambulika. Namna haitambuliki. Kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Yanasemwa hayohayo kuhusu Kushuka:
”Kushuka chini si kitu kisichofahamika. Namna haitambuliki. Kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Kanuni hii inapaswa kutumika katika sifa zote. Waarabu wanajua maana ya Sifa hizi. Hata hivyo sifa za Muumba ni kamilifu zaidi, tukufu zaidi na kuu mno kusema zilinganishwe na chochote katika sifa za viumbe. Kama ambavo dhati ya Muumba (Jalla wa ´Alaa) ni haki, viumbe pia wako na dhati. Dhati ya Muumba (Jalla wa ´Alaa) ni kamilifu, takasifu na tukufu zaidi kuweza kulinganishwa na chochote katika dhati za viumbe.”[3]
Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake wote.
[1] 20:05
[2] Twariyq-ul-Wusuul ilaal-´Ilm al-Ma’muul, uk. 8.
[3] Manhaj wa Diraasaat li Aayaat-il-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 21
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 84-85
- Imechapishwa: 18/12/2025
3 – Shaykh na ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Imaam Maalik na wengineo katika Salaf waliulizwa kuhusiana na maneno Yake (Ta’ala):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]
Amelingana juu vipi?” Akajibu: “Kulingana juu kunatambulika na namna haitambuliki, ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah.” Akabainisha kuwa Kulingana juu kunajulikana na kwamba namna yake haitambuliki. Hayohayo ndio yanatakiwa kusemwa juu ya yale yote ambayo Allaah amejisifu Mwenyewe.”[2]
4 – Shaykh na ´Allaamah Muhammad al-Amiyn ash-Shanqwiytwiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Unapaswa kutambua ya kwamba watu wengi wanasema kwamba Aayah zinazohusiana na sifa haziko wazi. Hili ni kosa kwa upande mmoja na inawezekana kwa upande mwingine, kama alivyobainisha Imaam Maalik bin Anas. Maana zinajulikana kwa waarabu. Imaam Maalik amesema:
”Kulingana juu kunatambulika. Namna haitambuliki. Kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Yanasemwa hayohayo kuhusu Kushuka:
”Kushuka chini si kitu kisichofahamika. Namna haitambuliki. Kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Kanuni hii inapaswa kutumika katika sifa zote. Waarabu wanajua maana ya Sifa hizi. Hata hivyo sifa za Muumba ni kamilifu zaidi, tukufu zaidi na kuu mno kusema zilinganishwe na chochote katika sifa za viumbe. Kama ambavo dhati ya Muumba (Jalla wa ´Alaa) ni haki, viumbe pia wako na dhati. Dhati ya Muumba (Jalla wa ´Alaa) ni kamilifu, takasifu na tukufu zaidi kuweza kulinganishwa na chochote katika dhati za viumbe.”[3]
Swalah na amani zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake wote.
[1] 20:05
[2] Twariyq-ul-Wusuul ilaal-´Ilm al-Ma’muul, uk. 8.
[3] Manhaj wa Diraasaat li Aayaat-il-Asmaa’ was-Swifaat, uk. 21
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 84-85
Imechapishwa: 18/12/2025
https://firqatunnajia.com/63-daima-jibu-ni-lilelile/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket