62. Mshirikina analazimishwa kukubali ushirikina wake

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtu anaweza vilevile kumwambia: “Maneno yako, kwamba shirki ni kuabudu [tu] masanamu; je unamaanisha ya kwamba shirki imekomeka kwa jambo hili na kwamba kuwategemea watu wema na kuwaomba hayaingii katika hilo [shirki]?” Anaraddiwa na yale aliyoyataja Allaah katika Kitabu Chake kuhusu kukufuru kwa wale ambao wanawategemea Malaika, ´Iysaa na watu wema. Lazima akukubalie ya kwamba mwenye kumshirikisha katika ´ibaadah ya Allaah miongoni kwa watu wema, ndio shirki iliyotajwa kwenye Qur-aan – na ndilo lililokuwa likitarajiwa.

MAELEZO

Hili ndio jibu la pili. Unamaanisha ya kwamba shirki imekomeka kwa matendo haya na kwamba haijumuishi kuwategemea na kuwaomba watu wema? Hili linakadhibishwa na Qur-aan. Hana budi kukukubalia ya kwamba yule mwenye kumuabudu mtu mwema anaingia katika shirki iliyotajwa katika Qur-aan, na hili ndilo lililokuwa likitarajiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 74
  • Imechapishwa: 25/11/2023