62. Kuna matishio gani juu ya mke akiomba kuachika bila udhuru?

Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote atakayemuomba mumewe talaka pasi na sababu basi ni haramu juu yake harufu ya Pepo.”

Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na akaifanya kuwa nzuri na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

Hayo ni kwa sababu talaka ndio kitu kinachochukizwa zaidi kwa Allaah. Talaka inaendewa wakati wa haja. Pasi na haja imechukizwa kutokana na yale madhara yanayopelekea yanayojulikana. Haja ambayo inaweza kumfanya mwanamke kuomba talaka ni pale ambapo atakataa kumtekelezea haki zake kwa njia ya kwamba mwanamke anadhurika kwa kuendelea kubaki pamoja naye. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ

“Hivyo kuzuia kwa mujibu wa Shari´ah au kuachia kwa wema.”[1]

لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

”Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao [kutokujamiiana] basi wangojee miezi minne. Wakirejea, basi hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.”[2]

[1] 02:229

[2] 02:226-227

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 110
  • Imechapishwa: 26/11/2019