Mtume huleta Takbiyr wakati anapoinua kichwa chake kutoka katika Sujuud[1] na alimwamrisha kufanya hivo yule mwanamume aliyeswali kimakosa:

“Haitimii swalah ya mtu yeyote mpaka… halafu asujudu kwa utulivu mpaka kila mfupa utue mahala pake kisha aseme:

الله اكبر

“Allaah ni mkubwa.”[2]

Baada ya hapo ainue kichwa chake mpaka aketi akiwa amenyooka.”

Wakati fulani (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akinyanyua mikono yake sambamba na Takbiyr hii[3].

Halafu akiutandaza mguu wake wa kushoto akiukalia kwa kutulizana[4]. Alimwamrisha kufanya hivo yule mtu aliyeswali kimakosa na kusema:

“Unaposujudu basi jimakinishe kwa Sujuud yako. Unapoinuka kalia paji lako la kushoto.”[5]

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiusimamisha mguu wake wa kushoto[6] na akivipindisha vidole vya miguuni kuelekea Qiblah[7].

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Daawuud na al-Haakim aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[3] Ahmad na Abu Daawuud kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh. Ahmad alikuwa akionelea kuwa mikono inatakiwa kunyanyuliwa sawa wakati wa Takbiyr hii na nyenginezo.” Ibn-ul-Qayyim amesema:

“al-Athram amepokea ya kwamba aliulizwa kuhusu kunyanyua mikono ambapo akajibu: “Kwa kila kwenda chini na juu.” al-Athram amesema: “Nilimuona Abu ´Abdillaah akinyanyua mikono kwa kila wakati anapoenda chini na juu.” (al-Badaa-iy (04/89))

Haya ndio maoni pia ya Ibn-ul-Mundhir na Abu ´Aliy kutoka katika Shaafi´iyyah. Vilevile ndio maoni ya Maalik na ash-Shaafi´iy, kama ilivyotajwa katika “Tarh-uth-Tathriyb”. Unyanyuaji mikono huu umesimuliwa kwa usahihi kutoka kwa Anas, Ibn ´Umar, Twaawuus, al-Hasan al-Baswriy, Ibn Siyriyn na Ayyuub as-Sikhtiyaaniy, kama ilivyotajwa kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh katika “al-Muswannaf” (01/106) ya Ibn Abiy Shaybah.

[4] al-Bukhaariy katika ”Juz’ Raf´-il-Yadayn”, Abu Daawuud kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh, Muslim na Abu ´Awaanah. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (316).

[5] Abu Daawuud na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[6] al-Bukhaariy na al-Bayhaqiy.

[7] an-Nasaa’iy kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 07/08/2017