al-´Ayyaashiy amesema:
“Rifaa´ah bin Musaa ameeleza ya kwamba alimsikia Abu ´Abdillaah akisema kuhusiana na Aayah:
وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا
“Amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende.”[1]
“Atapojitokeza al-Qaa´im[2] hakuna nchi yoyote isipokuwa kutanadiwa shahaadah.”[3]
Ametaja mapokezi mawili ambapo moja wapo unafungamanisha Aayah na ´Aliy na mwingine unafungamanisha Aayah na al-Qaa´im. Huu ni upotoshaji mbaya kabisa na ni kucheza na maana ya Qur-aan na makusudio yake makubwa. Namna hii ndio ilivyo maana ya Aayah: Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:
“Allaah (Ta´ala) anasema hali ya kumkemea ambaye anataka dini nyingine isiyokuwa dini ya Allaah ambayo kwayo ametuma Vitabu Vyake na kutuma Mitume Wake; dini ambayo ´ibaadah zote zinatakiwa kuelekezewa Allaah Pekee ambaye vimejisalimisha Kwake vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Ina maana kwamba vimejisalimisha Kwake sawa kwa kupenda au kutokupenda. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا
“Kwa Allaah pekee humsujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini kwa khiyari na kwa kuchukia.”[4]
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ
“Je, hawaoni vile alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinaelemea kulia na kushoto vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea? Kwa Allaah pekee vinamjusudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo na Malaika – nao hawatakabari; wanamwogopa Mola wao Aliye juu yao na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[5]
Muumini ni mwenye kujisalimisha kwa khiyari ilihali kafiri ni mwenye kujisalimisha kwa kutenzwa nguvu na kwa ajili hiyo anakuwa chini ya uendeshwaji, mamlaka na ufalme mkubwa ambao hawezi kwenda kinyume nao wala kupinzana nao.”[6]
Hii ndio tafsiri ya haki. Tazama tafsiri hii ni Tawhiyd maana iliyoje yenye nuru na tukufu ilio nayo. Kisha linganisha tafsiri hiyo na tafsiri ya huyu Raafidhwiy Baatwiniy uone namna ambavyo maadui wa Allaah, Mtume Wake na Maswahabah zake wanavyocheza na Kitabu cha Allaah na maana yake.
[1] 03:83
[2] al-Mahdiy.
[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/183).
[4] 13:15
[5] 16:48-50
[6] Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/102).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 100
- Imechapishwa: 03/04/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 100
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/62-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-sita-wa-aal-imraan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)