Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

52 – Yule mwenye kumsifu Allaah kwa njia ya kimtu basi amekufuru.

53 – Yule mwenye kuyazingatia haya basi atapata mazingatio, kukomeka na ´Aqiydah ya makafiri na atatambua kuwa sifa Zake hazifanani na sifa za watu.

MAELEZO

Bi maana ambaye atamfananisha Allaah na mtu amekufuru kwa sababu atakuwa amemsifu Allaah (´Azza wa Jall) kwa mapungufu.

Kwa sababu kuna tofauti ya wazi kati ya sifa za Muumba na sifa za viumbe, ijapo kuna ushirikiano kati ya majina na maana. Hata hivyo uhalisia na uhakika wake unatofautiana. Kwa hivyo maneno ya Allaah hayafanani na maneno ya mtu. Usikizi wa Allaah haufanani na usikizi wa mtu. Uoni wa Allaah haufanani na uoni wa mtu. Ujuzi wa Allaah haufanani na ujuzi wa mtu. Matakwa ya Allaah hayafanani na matakwa ya mtu. Kuna tofauti kati ya sifa za Allaah na sifa za viumbe. Yule asiyetofautisha kati yazo ni kafiri.

Yule ambaye atazingatia Aayah za Qur-aan ambazo Allaah ameziteremsha kwa al-Waliyd bin al-Mughiyrah basi atatambua upotofu wa mapote haya yaliyopotea kuhusiana na maneno ya Allaah (´Azza wa Jall). Sifa za Allaah, kukiwemo maneno Yake, zinatofautiana na sifa za watu kwa sababu sifa za Muumba zinatofautiana na sifa za viumbe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 71-72
  • Imechapishwa: 12/01/2023