Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Ama kuhusu:
اللهم بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على إبراهيم و على آل إبراهيم، إنك حميد مجيد
”Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa na Mwenye kutukuzwa.”
na yanayokuja baada yake, yanazingatiwa kuwa ni katika maneno na matendo yaliyopendekezwa.
MAELEZO
Maana ya maneno haya ni kwamba kusoma Tashahhud na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo la lazima. Ama kusema:
اللهم بارك على محمد
”Ee Allaah! Mbariki Muhammad… ”
na yanayokuja baada yake miongoni mwa Dhikr na kukaa kwa ajili ya Dhikr hiyo ni Sunnah za kimaneno na za kivitendo. Sunnah za kimaneno na za kivitendo ndani ya swalah ni nyingi. Zimetajwa katika vitabu vya Fiqh kikiwemo kitabu “Daliyl-ut-Twaalib”, uk. 35 cha Mar’iy bin Yuusuf.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 87
- Imechapishwa: 05/07/2026
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Ama kuhusu:
اللهم بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على إبراهيم و على آل إبراهيم، إنك حميد مجيد
”Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa na Mwenye kutukuzwa.”
na yanayokuja baada yake, yanazingatiwa kuwa ni katika maneno na matendo yaliyopendekezwa.
MAELEZO
Maana ya maneno haya ni kwamba kusoma Tashahhud na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo la lazima. Ama kusema:
اللهم بارك على محمد
”Ee Allaah! Mbariki Muhammad… ”
na yanayokuja baada yake miongoni mwa Dhikr na kukaa kwa ajili ya Dhikr hiyo ni Sunnah za kimaneno na za kivitendo. Sunnah za kimaneno na za kivitendo ndani ya swalah ni nyingi. Zimetajwa katika vitabu vya Fiqh kikiwemo kitabu “Daliyl-ut-Twaalib”, uk. 35 cha Mar’iy bin Yuusuf.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 87
Imechapishwa: 05/07/2026
https://firqatunnajia.com/61-kuanzia-hapa-ni-sunnah-za-kimaneno-na-kivitendo/