Hapa kunafuatia baadhi ya mifano ambayo wanazuoni wameyazingatia masimulizi haya kuwa ni kanuni moja wapo miongoni mwa kanuni za majina na sifa za Allaah:
1 – Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
“Iwapo mtu atauliza vipi Amelingana juu ya ´Arshi, atajibiwa kama alivosema Rabiy’ah, Maalik na wengineo (Radhiya Allaahu ‘anhum): “Kulingana juu kunatambulika, namna haitambuliki, ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza namna yake ni Bid´ah. Kwa sababu ni kuuliza kuhusu kitu asichokitambua mtu na wala hawawezi kulijibu.
Vivyo hivyo inapokuja mtu akiuliza ni namna gani Allaah anavyoshuka kwenye mbingu ya chini kabisa ya ulimwengu. Jawabu ni: Yeye yukoje? Ikiwa muulizaji atasema kwamba yeye hajui namna Alivyo, basi nasi hatujui namna ya kushuka Kwake. Kwa sababu ili mtu awe na utambuzi wa namna ilivyo sifa kunapelekea kuwa na utambuzi wa namna alivyo yule Msifiwa. Mawili hayo hayaachani. Ni vipi basi unanitaka kuwa na utambuzi wa namna Anavyosikia, anavyoona, maneno Yake, kulingana Kwake na kushuka Kwake ilihali hujui namna ilivyo dhati Yake?”[1]
Amesema tena (Rahimahu Allaah):
“Yeyote anayefasiri Kulingana juu (الإستواء) kwamba ni kutawala (الإستيلاء) amejibu kinyume na alivyojibu Maalik (Rahimahu Allaah) na kushika njia isiyokuwa njia yake. Jibu la Maalik (Rahimahu Allaah) kuhusu Kulingana juu ni lenye kutosha juu ya sifa nyengine zote, kama vile Ushukaji, Ujio, Mkono na Uso. Kwa mfano mtu anatakiwa kusema kuhusu Ushukaji:
”Kushuka chini kunatambulika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na ni kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Vivyo hivyo inatakiwa kusemwa juu ya sifa nyingine zote, kwa sababu zinalingana na Kulingana juu ambako kumetajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah.”[2]
[1] at-Tadmuriyyah, uk. 21.
[2] Majmuu´-ul-Fataawaa (4/4).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 82-83
- Imechapishwa: 17/12/2025
Hapa kunafuatia baadhi ya mifano ambayo wanazuoni wameyazingatia masimulizi haya kuwa ni kanuni moja wapo miongoni mwa kanuni za majina na sifa za Allaah:
1 – Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):
“Iwapo mtu atauliza vipi Amelingana juu ya ´Arshi, atajibiwa kama alivosema Rabiy’ah, Maalik na wengineo (Radhiya Allaahu ‘anhum): “Kulingana juu kunatambulika, namna haitambuliki, ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza namna yake ni Bid´ah. Kwa sababu ni kuuliza kuhusu kitu asichokitambua mtu na wala hawawezi kulijibu.
Vivyo hivyo inapokuja mtu akiuliza ni namna gani Allaah anavyoshuka kwenye mbingu ya chini kabisa ya ulimwengu. Jawabu ni: Yeye yukoje? Ikiwa muulizaji atasema kwamba yeye hajui namna Alivyo, basi nasi hatujui namna ya kushuka Kwake. Kwa sababu ili mtu awe na utambuzi wa namna ilivyo sifa kunapelekea kuwa na utambuzi wa namna alivyo yule Msifiwa. Mawili hayo hayaachani. Ni vipi basi unanitaka kuwa na utambuzi wa namna Anavyosikia, anavyoona, maneno Yake, kulingana Kwake na kushuka Kwake ilihali hujui namna ilivyo dhati Yake?”[1]
Amesema tena (Rahimahu Allaah):
“Yeyote anayefasiri Kulingana juu (الإستواء) kwamba ni kutawala (الإستيلاء) amejibu kinyume na alivyojibu Maalik (Rahimahu Allaah) na kushika njia isiyokuwa njia yake. Jibu la Maalik (Rahimahu Allaah) kuhusu Kulingana juu ni lenye kutosha juu ya sifa nyengine zote, kama vile Ushukaji, Ujio, Mkono na Uso. Kwa mfano mtu anatakiwa kusema kuhusu Ushukaji:
”Kushuka chini kunatambulika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na ni kuuliza juu yake ni Bid´ah.”
Vivyo hivyo inatakiwa kusemwa juu ya sifa nyingine zote, kwa sababu zinalingana na Kulingana juu ambako kumetajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah.”[2]
[1] at-Tadmuriyyah, uk. 21.
[2] Majmuu´-ul-Fataawaa (4/4).
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 82-83
Imechapishwa: 17/12/2025
https://firqatunnajia.com/61-jibu-kama-alivosema-maalik/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket