Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwani hawa waliotajwa mwisho ni warithi wa Mitume, makhaliyfah wa Mitume na viongozi wa uongofu ambao Qur-aan imesimama kupitia wao na wakaitendea kazi. Qur-aan imetamka kupitia wao na wakazungumza kwa mujibu wake. Allaah amewatunuku elimu na hekima ambavyo kwavyo wamewashinda wafuasi wa Mitume wengine wote, sembuse nyumati nyengine zisizokuwa na kitabu. Wamezizunguka elimu ambazo wengine wangelistahi kukabilishwa na wao.
MAELEZO
Ni vipi hawa waliokuja nyuma watakuwa bora kuliko Salaf ambao miongoni mwa sifa yao kubwa ni kwamba wao ni warithi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam)? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Wanazuoni ndio warithi wa Mitume. Hakika Mitume hawakuacha dinari wala dirhamu. Hakika hapana vyenginevo wameacha elimu.”[1]
Inatosha kuwa heshima ya kwamba wanazuoni ndio warithi wa Mitume. Elimu ya Shari´ah ambayo wamekuja nayo Mitume ndio inayowafakhirisha. Elimu hiyo ndio kheri na uongofu duniani na Aakhirah. Kuhusu ambaye ameichukua elimu yake kutoka kwa wanafalsafa, watu wa mantiki na wafikiriaji na si kutoka kwa Mitume, hakurithi kheri yoyote – amerithi uovu, shaka, mkanganyiko na kusitasita.
Salaf ndio makhaliyfah wa Mitume katika kueneza elimu na kulingania kwa Allaah. Mwanazuoni ni khaliyfah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) duniani inapokuja katika kueneza na kuifunza elimu, kulingania kwa Allaah, kuamrisha mema na kukataza maovu. Huyu ndiye khaliyfah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu ambaye yuko na elimu lakini hasimamii wajibu wake si katika makhaliyfah wa Mitume kabisa. Huyu hakuna kingine alichofanya isipokuwa yale aliyoyahifadhi ni hoja dhidi yake. Anaingia miongoni mwa wale walioficha elimu na hawasimami kwayo. Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ
“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja za wazi na mwongozo baada ya kuwa tumeyabainisha kwa watu ndani ya Kitabu, hao anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.”[2]
Pamoja na kwamba ni wanazuoni, lakini pale walipoificha elimu Allaah akawalaani na wakalaaniwa na kila mwenye kulaani.
[1] Abu Daawuud (3641), at-Tirmidhiy (2682), Ibn Maajah (223) na Ahmad (5/196). Nzuri kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (70).
[2] 2:159
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 98-99
- Imechapishwa: 13/08/2024

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 98-99
Imechapishwa: 13/08/2024
https://firqatunnajia.com/60-salaf-walikuwa-warithi-wa-mitume/