Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Wamesimamisha Kitabu na Kitabu kikasimama kupitia wao.

MAELEZO

Bi maana waliibeba na kuitendea kazi Qur-aan. Kwa sababu ni lazima Qur-aan ipate wenye kuibeba. Amesema (Ta´ala):

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ

“Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo kusomwa kwake.”[1]

Si kama wanavyofikiria baadhi ya watu ya kwamba inahusiana na Tajwiyd, kuisoma kwa vigezo vyake vyote na kuitamka sahihi ipasavyo. Hayo ni namna ya usomaji wake, kwa haki ipasavyo ni kule kutambua maana yake na kuitendea kazi. Ama kuhusu elimu ya Tajwiyd ni njia tu – na si lengo – ya kuisoma vizuri ikiwa mtu hakuchupa mipaka katika jambo hilo.

Kitabu kimetamka kupitia wao kwa njia ya kwamba kimewasifu na kuwataja. Wametamka kwa mujibu wa Kitabu kwa njia ya kwamba hawakutamka isipokuwa kwa yale yaliyojulishwa na Qur-aan. Yale yaliyojulishwa na Qur-aan, waliyatamka, na yale ambayo hayakujulishwa na Qur-aan, waliyanyamazia.

[1] 2:121

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 99
  • Imechapishwa: 13/08/2024