7 – Sifa za wanazuoni kwake:

1- ash-Shafi’iy amesema:

“Elimu inazunguka kwa watu watatu: Maalik, al-Layth na Ibn ´Uyaynah.”

2 – Imepokewa kwamba al-Awzaa’iy alikuwa akisema wakati anapomtaja Maalik:

“Mwanachuoni wa wanazuoni na muftiy wa misikiti miwili Mitakatifu.”

3 – Baqiyyah amesema:

“Hakukubaki juu ya uso wa ardhi ambaye ni mjuzi zaidi wa Sunnah kuliko wewe, ee Maalik.”

4 – Abu Yuusuf amesema:

“Sijaona mtu yeyote mjuzi zaidi kuliko Abu Haniyfah, Maalik na Ibn Abiy Laylaa.”

5 – Ahmad bin Hanbal alimtaja Maalik, akamtanguliza mbele ya al-Awzaa’iy, ath-Thawriy, al-Layth, Hammaad na al-Hakam ilipokuja katika suala la elimu na akasema:

“Yeye ni Imaam katika Hadiyth na Fiqh.”

6- al-Qattwaan amesema:

“Yeye ni imamu anayefuatwa.”

7-  Ibn Ma’iyn amesema:

“Maalik ni katika hoja za Allaah dhidi ya viumbe Wake.”

8- Asad bin al-Furaat amesema:

“Ikiwa mnamtafuta Allaah na Aakhirah, basi shikamaneni na Maalik.”

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 15
  • Imechapishwa: 27/11/2025