al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri:
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ
“[Kumbukeni pindi] Allaah alipochukua fungamano kwa Manabii [akawaambia:] “Nikisha kupeni Kitabu na hikmah, kisha [siku moja] akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mlionayo; ni juu yenu mumuamini na mumnusuru.”[1]
“Habiyb as-Sijistaaniy amesema: “Nilimuuliza Abu Ja´far juu ya maneno ya Allaah:

“[Kumbukeni pindi] Allaah alipochukua fungamano kwa Manabii [akawaambia:] “Nikisha kupeni Kitabu na hikmah, kisha [siku moja] akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mlionayo; ni juu yenu mumuamini na mumnusuru.”
Ni vipi Muusa atamuamini na kumnusuru ´Iysaa ilihali hakukutana nae? Ni vipi ´Iysaa atamuamini na kumnusuru Muhammad ilihali hakukutana nae?” Akajibu: “Ee Habiyb! Kuna mengi yameondoshwa kwenye Qur-aan na hakuna kilichowekwa isipokuwa makosa ya waandishi ambayo watu wanafikiria kuwa ni ya sawa. Ni kosa. Isome namna hii:
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ امم النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ
“[Kumbukeni pindi] Allaah alipochukua fungamano kwa nyumati za Manabii [akawaambia:] “Nikisha kupeni Kitabu na hikmah, kisha [siku moja] akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mlionayo; ni juu yenu mumuamini na mumnusuru.”[2]
Namna hii ndivyo ilivyoteremshwa, ee Habiyb! Ninaapa kwa Allaah kwamba hakuna Ummah wowote kabla ya Muusa uliotekeleza fungamano ambalo Allaah alichukua kwao. Ummah uliojiwa na Muusa ulimkanusha ´Iysaa isipokuwa wachache tu. Ummah wa ´Iysaa haukumuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala haukumnusuru isipokuwa wachache tu. Ummah huu ulikanusha fungamano ambalo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichukua kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) pindi alipomteua kwa watu na akawaomba kusimama bega kwa bega na yeye na kumnusuru. Akawaomba washuhudie hilo juu ya nafsi zao. Ni fungamano lipi muhimu zaidi kama uteuzi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumteua ´Aliy bin Abiy Twaalib? Ninaapa kwa Allaah kwamba hawakulitekeleza. Walikanusha na wakakadhibisha.”[3]
Hata mayahudi na manaswara hawakufikia kumsemea uongo Allaah, Kitabu Chake na Mtume Wake kama walivyofanya Baatwiniyyah Raafidhwah. Ni nani aliyeondosha kutoka katika Qur-aan Aayah nyingi? Maadui wa Allaah Baatwiniyyah wanawalenga Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na khaswa Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum).
´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliishi miaka thelathini baada ya kufa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawa kiongozi wa waumini. Uongozi wake ulitapakaa katika nchi nyingi za Kiislamu kutokea Iraak kufika mpaka Khuraasaan, kutoka Hijaaz mpaka Misr na Yemen. Ni kipi kilichomzuia kusema kuwa sehemu kubwa ya Qur-aan iliondoshwa? Yeye si alikuwa ni shujaa mkubwa na majeshi nyuma yake. Ni kipi kilichomzuia kuonyesha msahafu kamilifu unaodaiwa na Raafidhwah Baatwiniyyah na kwamba waliondosha mengi katika Qur-aan na kwamba ´Aliy na familia yake wana msahafu kamilifu na hawakuwawekea nao watu hadharani ili wauamini na wautendee kazi, hakuna Ummah wowote uliojua mazuio haya makubwa na khiyana hii mbaya kama mfano huu! Hata hivyo hakuna uwezekano wowote haya yakawa yamesihi kwa ´Aliy na familia yake. Mpango wa Raafidhwah kwa haya ni ´Aliy na familia yake watuhumiwe khiyana, maficho na woga kama ambavyo wanawakufurisha Maswahabah na kuwatuhumu kuzidisha na kupunguza katika Qur-aan.
[1] 03:81
[2] 03:81
[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/180-181).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 94-95
- Imechapishwa: 03/04/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 94-95
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/59-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-tano-wa-aal-imraan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)