Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa kumi

Kuwategemea watu wema ni shirki

Akisema: “Simshirikishi Allaah na chengine chochote, kamwe, lakini kuwaelekea watu wema sio shirki”. Mwambie: “Ukiwa kweli unakubali ya kwamba Allaah ameharamisha shirki na kwamba ni jambo kubwa kuliko zinaa na unakubali ya kwamba Allaah hatoisamehe, ni jambo gani sasa ambalo Allaah kaharamisha na kasema kwamba hatolisamehe?” Kwa hakika hajui.

MAELEZO

Mshirikina akisema kuwa yeye hamshirikishi Allaah na chochote na kwamba kuwaelekea watu wema sio shirki, mwambie yafuatayo:

“Je, wewe hukubali ya kwamba Allaah ameharamisha shirki zaidi kuliko alivyoharamisha zinaa? Unakubaliana na mimi kuwa Allaah haisamehi? Shirki hii ni ipi?”

Hatojua na wala hatojibu kisawasawa muda wa kuwa anaonelea kuwa kumuomba uombezi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sio shirki. Ni dalili yenye kuonyesha kuwa hajui shirki ni kitu gani. Allaah (Ta´ala) amesema juu yake:

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

“Hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” (31:13)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 72
  • Imechapishwa: 24/11/2023