4 – Abul-Ma´aaliy al-Juwayniy amesema:

”Miongoni mwa maneno mazuri ya Imaam Maalik wakati alipoulizwa ni namna gani Amelingana kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

akajibu:

“Kulingana juu kunatambulika na namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini jambo hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah.”

Namna hiyohiyo ndio zinatakiwa kukabiliwa Aayah ya Kulingana juu, Ujio, Aayah nyenginezo kama vile:

مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

”Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa mikono Yangu?”[2]

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ

”… na utabakia uso wa Mola wako.”[3]

تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا

”Inatembea chini ya macho Yetu.”[4]

na yale yaliyosihi kuhusiana na masimulizi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), kama vile Kushuka.”[5]

[1] 20:05

[2] 38:75

[3] 55:27

[4] 54:14

[5] al-´Aqiydah an-Nidhwaamiyyah, uk. 25. Lakini Abul-Ma´aaliy ameegemea katika kijitabu chake hichi kwenye kutegemeza (التفويض) maana. Hiyo ndio ´Aqiydah yake ya mwisho. Alidhani kuwa hiyo ndio ´Aqiydah ya Salaf, kama vile Maalik. Tazama “Dar’-ut-Ta´aarudhw” (5/249) ya Ibn Taymiyyah.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 81