57. Ni vipi watakuwa wajuzi zaidi kuliko Salaf?

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Ni vipi watu hawa ambao wamenyimwa, waliopungukiwa, waliotanguliwa na ambao wamedangana na kuwa na mashaka watakuwa wajuzi zaidi juu ya Allaah, majina na sifa Zake na wenye hekime zaidi inapokuja katika Aayah na dhati Yake kuliko wale waliotangulia mwanzoni awali ambao ni Mujaaruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema?

MAELEZO

Ni wapi wataitoa elimu hii ilihali wao hawajengei hoja kwa Qur-aan wala Sunnah. Wanajenga hoja kwa mifumo yao maalum waliyozuliwa na wanafalsafa wao na viongozi wao wa mijadala. Si jengine isipokuwa ni ujinga juu ya Allaah (´Azza wa Jall).

Hizi ndio sifa mbaya za wale waliokuja nyuma. Ni watu wamekuja nyuma inapokuja upande wa zama na inapokuja katika elimu na ufahamu. Wamechanganyikiwa. Kwa sababu hakuna elimu yao ilichowazidishia isipokuwa mikanganyiko na shaka. Haikuwazidishia uongofu. Ni vipi basi watu hawa watakuwa wajuzi zaidi kuliko Salaf ambao wameichukua elimu yao kutoka katika Qur-aan na Sunnah na wale waliovifikisha? Ukilinganisha kati ya Salaf na watu hawa, basi utaona tofauti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 95
  • Imechapishwa: 12/08/2024