3- Mwenye kuuliwa kwa kusimamishiwa adhabu miongoni mwa adhabu za Allaah. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Imraan bin Huswayn:

“Kuna mwanamke mmoja katika kabila la Juhaynah alimjia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na ujauzito wa uzinzi ambapo akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nimewajibikiwa na adhabu. Nitekelezee nayo!” Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwita walii wake akamwambia: “Mtendee wema. Akishazaa niletee naye. Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha azifunge vizuri nguo zake kisha akaamrisha apigwe mawe. Halafu baadaye akamswalia. ´Umar akasema kumwambia: “Je, hivi kweli unamswalia ilihali amezini?” Akasema: “Hakika ametubu tawbah ambayo ingegawanywa kati ya watu sabini wa al-Madiynah basi ingeliwaenea. Hivi kweli ipo tawbah bora kuliko yeye mwenyewe kujileta kwa Allaah (Ta´ala)?”

Ameipokea Muslim (05/121), Abu Daawuud (02/233), an-Nasaa´iy (01/278), at-Tirmidhiy (02/325) ambaye ameisahihisha. Pia ameipokea ad-Daarimiy (02/180), al-Bayhaqiy (04/18, 19) na Ibn Maajah (02/116,117) kwa mukhtasari.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 108
  • Imechapishwa: 16/07/2020