57. Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn wataingia Peponi

Vivyo hivyo Faatwimah, msichana wake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhum). Hudhayfah bin al-Yamaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mama yangu aliniuliza: “Ni lini ilikuwa kukutana kwako kwa mwisho?” Bi maana na Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nikasema kuwa tangu kitambo kidogo ambapo akanifokea. Nikasema: “Hebu wacha nende kwa Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), niswali pamoja naye Maghrib na kumuomba aniombee du´aa na wewe.” Nikaenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuswali pamoja naye Maghrib na baadaye nikaswali ´Ishaa pamoja naye. Kisha akashika njia yake ambapo nikamfuata. Akasikia sauti yake akasema: “Je, ni Hudhayfah?” Nikasema: “Ndio.” Akasema: “Una haja gani? Allaah akusamehe wewe na mama yako. Usiku huu kuna Malaika ambaye ilikuwa ndiye mara yake ya kwanza kushuka ulimwenguni. Amemuomba idhini Mola wake anisalimie na anipe khabari njema ya kwamba Faatwimah ndiye bibi wa wanawake wa Peponi na kwamba al-Hasan na al-Husayn ndiye mabwana wa vijana wa Peponi.”[1]

[1] Ahmad (5/391-392) na at-Tirmidhiy (3781). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3781).

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 137
  • Imechapishwa: 20/05/2026