Ahl-us-Sunnah wanawashuhudilia Pepo watu wengine ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwashuhudilia Pepo. Miongoni mwa watu hao ni ´Ukaashah bin Mihswan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Mtume akiwa na kundi dogo la watu, na Mtume akiwa na mtu mmoja au wawili, na Mtume akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaonyeshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: “Huyo ni Muusa na watu wake.” Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaambiwa: “Hawa ni watu wako, miongoni mwao kuna 70.000 watakaoingia Peponi bila ya kufanyiwa hesabu wala adhabu.” Kisha akainuka na kwenda nyumbani. Huku nyuma watu wakaanza kujadiliana ni nani hao watakaoweza kuwa? Baadhi yao wakasema: “Pengine ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).” Wengine wakasema: “Pengine ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah na chochote.” Wakataja mengine kadhaa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akatoka na kuja na wakamweleza waliyokuwa wakiyajadili. Akasema: “Ni wale wasioomba kusomewa Ruqyah, hawajichomi chuma cha moto na wala hawaamini rajua nzuri na mbaya, bali wanamtegemea Mola Wao.” ‘Ukaashah bin Mihswan (Radhiya Allaahu ‘anh) aliposikia alisimama akasema: “Muombe Allaah anijaalie kuwa mmoja wao.” Akasema: “Wewe ni katika wao.” Kisha akasimama mtu mwengine na kusema: “Muombe Allaah anijaalie kuwa mmoja wao.” Akasema: “´Ukaashah amekutangulia.”[1]
[1] al-Bukhaariy (5705) na Muslim (220).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 135-136
- Imechapishwa: 20/05/2026
Ahl-us-Sunnah wanawashuhudilia Pepo watu wengine ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwashuhudilia Pepo. Miongoni mwa watu hao ni ´Ukaashah bin Mihswan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ummah zote zilipitishwa mbele yangu, nikamuona Mtume akiwa na kundi dogo la watu, na Mtume akiwa na mtu mmoja au wawili, na Mtume akiwa hana mtu yeyote. Kisha nikaonyeshwa idadi kubwa ya watu niliodhania ni katika Ummah wangu, lakini nikaambiwa: “Huyo ni Muusa na watu wake.” Kisha nikatazama nikaona kundi kubwa ambalo nikaambiwa: “Hawa ni watu wako, miongoni mwao kuna 70.000 watakaoingia Peponi bila ya kufanyiwa hesabu wala adhabu.” Kisha akainuka na kwenda nyumbani. Huku nyuma watu wakaanza kujadiliana ni nani hao watakaoweza kuwa? Baadhi yao wakasema: “Pengine ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).” Wengine wakasema: “Pengine ni wale waliozaliwa katika Uislamu na hawakumshirikisha Allaah na chochote.” Wakataja mengine kadhaa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akatoka na kuja na wakamweleza waliyokuwa wakiyajadili. Akasema: “Ni wale wasioomba kusomewa Ruqyah, hawajichomi chuma cha moto na wala hawaamini rajua nzuri na mbaya, bali wanamtegemea Mola Wao.” ‘Ukaashah bin Mihswan (Radhiya Allaahu ‘anh) aliposikia alisimama akasema: “Muombe Allaah anijaalie kuwa mmoja wao.” Akasema: “Wewe ni katika wao.” Kisha akasimama mtu mwengine na kusema: “Muombe Allaah anijaalie kuwa mmoja wao.” Akasema: “´Ukaashah amekutangulia.”[1]
[1] al-Bukhaariy (5705) na Muslim (220).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 135-136
Imechapishwa: 20/05/2026
https://firqatunnajia.com/55-ukaashah-bin-mihswan-ataingia-peponi/