Hapana shaka yoyote kwamba masimulizi ya Imaam Maalik bin Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ni sahihi, yamethibiti, mazuri na yenye nguvu. Wanazuoni wameyapokea kwa kuyakubali, kuyaona ni mazuri na kuyajumuisha katika majibu mazuri na bora kabisa yaliyojibiwa juu ya maudhui haya. Wameyafanya kuwa ni kanuni miongoni mwa kanuni inapokuja katika majina na sifa za Allaah; inayotumiwa katika sifa zote. Kunasemwa juu ya kila sifa yale yaliyosemwa na Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) kuhusu sifa ya Kulingana. Tayari tumekwishatangulia katika mlango wa kujitegemea ambapo tumethibitisha vyanzo na kuthibiti kwake kutoka kwa Imaam Maalik (Rahimahu Allaah).

Katika mlango huu nitanukuu mambo mawili:

1 – Baadhi ya nukuu za wanazuoni juu ya uzuri wake na kuyasifu.

2 – Baadhi ya nukuu zinazoyazingatia maneno hayo kuwa ni kanuni moja wapo inapokuja katika majina na sifa za Allaah.

Inapokuja kwenye maneno ya wanazuoni ambapo wameyaonelea kuwa ni mazuri ya kuyakubali masimulizi haya, ni mengi mno. Kwa ajili hiyo ni mara chache mno kwamba utakosa ndani ya vitabu vya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kuyataja masimulizi haya, kuyajengea hoja na kuyasifu. Hapa kunafuatia baadhi ya mifano ya wale waliofanya hivo:

1 – Imaam Abu Sa´iyd ad-Daarimiy amesema:

“Maalik amesema kweli. Namna haitambuliki na Kulingana juu si kwamba ni kitu kisichotambulika. Qur-aan imetaja baadhi ya mambo hayo katika Aayah nyingi.”[1]

[1] ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 56.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 16/12/2025