Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Katika kuamini siku ya Aakhirah kunaingi kuyaamini yote aliyoelezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya yatakayokuwa baada ya mauti. Wanaamini mitihani ya ndani ya kaburi, adhabu ya kaburi na neema zake. Kuhusu mitihani yake ni kwamba watu watapewa mitihani ndani ya makaburi yao. Kila mtu ataulizwa ni nani Mola wako, ni ipi dini yako na ni nani Mtume wako[1]:
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ
”Allaah huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.” (14:27)
Muumini atasema: “Allaah ndio Mola Wangu, Uislamu ndio dini yangu na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio Mtume wangu.” Ama mwenye mashaka atasema: “Aah! Aah! Sijui. Nilisikia watu wanasema kitu na mimi nikakisema.” Hivyo atapigwa chuma cha Moto na atapiga kelele ya juu kabisa ambayo itasikiwa na viumbe vyote isipokuwa binaadamu. Na lau binaadamu aingeliisikia, basi angelizimia[2].
MAELEZO
Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah vilevile ni kuamini yale yote aliyoelezea Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa ni pamoja vilevile na mambo ya Aakhirah, Pepo, Moto, kufanyiwa hesabu na malipo. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini yote haya.
Miongoni mwa hayo kunaingia pia kuamini adhabu na neema za ndani ya kaburi. Ahl-us-Sunnah wanaamini hayo. Tofauti na Ahl-ul-Bid´ah. Ahl-us-Sunnah wanaamini adhabu na neema ya kaburi, kwamba watu watahojiwa ndani ya makaburi yao ambapo wataulizwa juu ya Mola, dini na Mtume Wao. Allaah huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti duniani na Aakhirah na madhalimu huwadhalilisha. Amesema (Subhaanah):
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖوَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ
“Allaah huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah; na Allaah huwaacha kupotoka madhalimu – na Allaah anafanya atakavyo.”
Muumini yeye atajibu kwa kusema kwamba Mola Wake ni Allaah, Uislamu ndio dini yake na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio Mtume Wake. Ama yule mwenye shaka na kafiri watasema kuwa hawajui. Hili linahusu mnafiki na kafiri. Huyu ni yule mnafiki ambaye alikuwa akidhihirisha Uislamu ilihali ni kafiri na kafiri anayeonyesha ukafiri waziwazi. Hawa ndio ambao watajibu kusema kuwa hawajui na kwamba walikuwa wakiwasikia watu wakisema kitu na wao wanasema. Atapigwa chuma cha moto na ukelele mkubwa ambao utasikia kila kiumbe isipokuwa mwanaadamu. Lau mwanaadamu angelisikia ukelele huo basi angelizimia.
[1] Abu Daawuud (4753) na at-Tirmidhiy (3120).
[2] ´Abdur-Razzaaq (6737), Abu Daawuud (4751), al-Bukhaariy (1338) na Muslim (2870).
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)