55. Ibn Taymiyyah kuhusu kumkufurisha anayemwomba asiye Allaah

Mtazamo wa pili katika mitazamo miwili iliyotangulia ni kukomeka kuhusiana na suala la kukufurisha ambayo yamethibitishwa na wanazuoni wengi akiwemo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ‘Abdul-Wahhaab. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu ”al-Istighaathah” (2/731):

“Basi hakika sisi baada ya kufahamu yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tunajua kwa yakini kuwa hakuwawekea katika Shari´ah ummah wake wamwombe yeyote katika wafu, si Mitume, waja wema wala mwengine – si kwa tamko la kuomba msaada wala jengine, si kwa tamko la kuomba kinga wala jengine. Kama ambavyo hakuwawekea katika Shari´ah ummah wake kumsujudia mfu wala asiye mfu na kadhalika. Bali tunajua kuwa aliyakataza mambo haya yote na kwamba hayo ni miongoni mwa ushirikina ambao Allaah na Mtume Wake wameuharamisha. Lakini kwa sababu ya kuenea kwa ujinga na uchache wa elimu ya athari ya nyujumbe kwa wengi miongoni mwa waliokuja baadaye, haikuwako kuwahukumu kuwa wamekufuru kwa hilo mpaka ibainike kwao yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na yale yaliyo kinyume nayo.  Kwa ajili hiyo sijawahi kubainisha suala hili kwa yeyote anayejua asili ya Uislamu isipokuwa atafahamu na kusema: “Hili ni asili ya dini.” Baadhi ya wakubwa katika Mashaykh wanaojua miongoni mwa watu wetu walisema: “Hili ndilo jambo kubwa kabisa ulilotubainishia” kwa sababu walijua kuwa hili ni msingi wa dini.”

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 01/07/2026