Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:
”Maadhimisho yote yanamstahiki Allaah kwa njia inayolingana na Ukubwa na Utukufu Wake, kama Rukuu´, Sujuud na kudumu milele.”
MAELEZO
´Ibaadah ni haki ya Allaah, kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall):
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
“Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.”[1]
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ
“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.””[2]
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ
“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”[3]
Kwa hiyo ni lazima kuelekeza aina zote za ´ibaadah kwa Allaah tu na haifai kuelekeza chochote katika ´ibaadah kwa mwingine asiyekuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Basi swalah ni kwa ajili ya Allaah, Rukuu’ na Sujuud ni kwa ajili ya Allaah, kuomba msaada wa dharura ni kwa Allaah, du´aa ni kwa Allaah, utegemezi ni kwa Allaah, kujikinga ni kwa Allaah na vivyo hivyo aina zote za ´ibaadah ni kwa ajili ya Allaah. Amesema (´Azza wa Jall):
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ
“Sema: “Hakika swalah yangu, kichinjwa changu, uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.”[4]
Yeyote mwenye kuelekeza chochote katika aina za ´ibaadah kwa asiyekuwa Allaah, basi huyo ni mshirikina na kafiri. Hukumu hii ni kwa ujumla na kwa yule ambaye amefikiwa na hoja. Kuhusu mtu maalum, ikiwa imetokea kwake kuelekeza chochote katika aina za ´ibaadah kwa asiye Allaah, kama vile kuomba wafu na kuwataka msaada ilihali ni mjinga, basi inazuilika kumkufurisha mpaka abainishiwe na asimamishiwe hoja. Huu ni mtazamo mojawapo katika mitazamo miwili juu ya suala hili, ambao umetajwa na Shaykh wetu ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) katika jibu la swali kuhusu baadhi ya wazushi. Imekuja ndani yake:
“Vilevile kufanya Tawassul kwa waja wema kumegawanyika aina mbili:
1 – Kufanya Tawassul kwa hadhi ya fulani au haki ya fulani. Hii ni Bida´ah na sio kufuru.
2 – Kumuomba kwa kusema ”Ee bwana fulani, nisaidie!” au ”Mponye mgonjwa wangu!”. Hii ni shirki kubwa ambayo pia wanaita kuwa ni Tawassul. Hii ni miongoni mwa matendo ya watu kabla ya kuja Uislamu. Lakini aina ya kwanza ni Bid´ah na ni miongoni mwa njia za shirki. Akaulizwa: ”Maneno yao wanaposema kwamba wao wanamwomba kwa sababu ni mja mwema na kila kitu kiko mikononi mwa Allaah na bwana huyu ni mkatikati tu?” Akajibu: ”Hiki ni kitendo cha watu wa kipindi kabla ya kuja Uislamu. Maneno yao: ”Tusaidieni, ee Badawiy!”, ”Tusaidieni, ee al-Husayn!” ni ya aina ya matendo ya Abu Jahl na mfano wake. Kwani wao wanasema:
مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ
“Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.”[5]
هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ
“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”[6]
Du´aa hii ni kufuru na shirki kwa Allaah (´Azza wa Jall). Lakini wanazuoni wamekhitalifiana kama mwenye kufanya hivo anatakiwa kukufurishwa au anasubiriwa hadi hoja isimamishwe dhidi yake na hadi abainishiwe kwanza?” Kuna mitazamo miwili:
1 – Kwamba anayesema haya ni kafiri mwenye aina ya ukafiri mkubwa, kwa sababu huu ni ushirikina wa wazi na dalili zake hazifichikani.
2 – Kwamba hawa wanaweza kuwa ni wajinga na wanafuata wanazuoni waovu waliowapoteza. Basi ni lazima waelezwe na kubainishiwa mpaka wajue, kwani Allaah amesema:
وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا
”Hatukuwa Wenye kuadhibu mpaka tumtume Mtume.”[7]
Pindi jambo litakapobainishwa kwao na wakaambiwa: “Hili halijuzu, kwa sababu Allaah amesema hivi na Mtume amesema hivi” wakaelezewa dalili, kisha wakang’ang’ania hali yao, wanakufuru kwa hilo. Katika hali zote, kitendo chenyewe ni ukafiri wa ushirikina mkubwa, lakini mwenye kitendo hicho ni mahali pa kuangaliwa: je, amekufuru au inasemwa kwamba jambo lake limo mikononi mwa Allaah? Huenda akawa miongoni mwa Ahl-ul-Fatrah kwa sababu jambo halikubainishwa kwake na hivyo hukumu yake huwa kama ya Ahl-ul-Fatrah. Jambo lake ni kwa Allaah, kwa sababu ya udanganyifu aliofanyiwa na watu kutokana na wanavyuoni wa uovu.”
Yamenukuliwa kutoka katika kitabu ”Sa´tu Rahmati Rabbil-´Aalamiyna lil-Juhhaal-il-Mukhaalifiyna lish-Shariy´ati minal-Muslimiyna” cha Sayyid bin Sa’dud-Diyn al-Ghabashiy. Mwanzoni mwa kitabu kuna barua kutoka kwa Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) iliyoandikwa tarehe 7/5/1403, inayohusisha kukubali kitabu hicho na kutoa idhini ya kuchapishwa kwake.
[1] 51:56
[2] 16:36
[3] 21:25
[4] 06:162-163
[5] 39:03
[6] 10:18
[7] 17:15
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 69-73
- Imechapishwa: 01/07/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 69-73
Imechapishwa: 01/07/2026
https://firqatunnajia.com/54-mitazamo-miwili-kuhusu-kumkufurisha-anayemwomba-asiye-allaah/