55. Hadiyth ”Hakuna watu watakaokaa kisha wakasimama… ”

55 – ´Aaswim bin ´Aliy, Hafsw bin ´Umar na Sulaymaan bin Harb wametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa Dhakwaan, kutoka kwa Abu Sa´iyd, ambaye amesema:

ما من قوم يقعدون ثم يقومون ولا يصلون على النبي صلى الله عليه وسلم إلا كان عليهم يوم القيامة حسرة، وإن دخلوا الجنة للثواب

”Hakuna watu watakaokaa kisha wakasimama pasi na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), isipokuwa siku ya Qiyaamah kitakuwa ni hasara hata kama ataingia Peponi kutokana na thawabu.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa njia ya maneno ya Swahabah, lakini ina hukumu moja kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na khaswa kwa kuzingatia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema namna hiyo. Imaam ameipokea na akasema: ´Abdur-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 54
  • Imechapishwa: 23/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy