55. Amemjamii mkewe ambaye amefunga swawm ya kulipa

Swali 55: Mume alirudi kutoka safarini ya muda mrefu ambapo akamkuta mke wake amefunga swawm ya kulipa. Hakuweza kujizuia ambapo akawa amemwingilia pasi na ridhaa yake. Ni kipi chenye kuwalazimu[1]?

Jibu: Ni wajibu kwake mume kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hilo linapaswa kuwa kwa kujutia kile alichokifanya na kuazimia kutokurudi katika jambo hilo kwa ajili ya kumuadhimisha Allaah na kutahadhari adhabu yake.

Kuhusu mwanamke ikiwa kweli alilazimishwa basi hakuna kinachomlazimu na swawm yake ni sahihi. Ama ikiwa alimchukulia wepesi basi ni lazima kwake kulipa siku hiyo na wala halazimiki kutoa kafara[2].

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/309-310).

[2] Tazama https://firqatunnajia.com/mume-amemwita-kitandani-katika-swawm-ya-kulipa-ramadhaan/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 78
  • Imechapishwa: 21/05/2022