55. al-Qummiy upotoshaji wake wa kwanza wa Aal ´Imraan

al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ

“Hakika Allaah amemteua Aadam na Nuuh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu wote.”[1]

“Matamshi ya Aayah ni yenye kuenea na maana yake ni maalum. Aliwafadhilisha juu ya walimwengu katika zama zao tu. Mwanachuoni amesema: “Kihakika inatakiwa iwe:

وَ آلَ عِمْرَانَ و آل محمد عَلَى الْعَالَمِينَ

“… ni kizazi cha ´Imraan na kizazi cha Muhammad juu ya walimwengu wote.”

Walitoa “kizazi cha Muhamma” kutoka kwenye Kitabu.”[2]

Mnamsemea uongo Allaah, Qur-aan, Abu ´Abdillaah, familia yake na maimamu. Hakuna yeyote aliyekanusha familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka Abu ´Abdillaah alazimishe kuthibitisha hilo katika Qur-aan. Haiwezekani kamwe akamzulia Allaah au Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Allaah na waislamu wote katika kila kizazi wanashuhudia ya kwamba ziada hii imetoka kwa mazanadiki katika Raafidhwah Baatwiniyyah. Halafu mazanadiki wanadai kuwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waaminifu (ambao Allaah kwao ameihifadhi Qur-aan na Ummah wa Kiislamu) wamepotosha Qur-aan!?!?

[1] 03:33

[2] Tafsiyr al-Qummiy (01/100).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 89
  • Imechapishwa: 03/04/2017