54. Radd kwa mwenye kudai kwamba kuwaomba du´aa na kinga watu wema sio ´Ibaadah

Akisema: “Mimi siabudu mwengine yeyote isipokuwa Allaah na huku kutafuta kinga kutoka kwao [watu wema] na kuwaomba [du´aa] sio ´Ibaadah”,

MAELEZO

Akitambua kuwa ´ibaadah ni haki ya Allaah (´Azza wa Jall) na kwamba haijuzu kumuabudu asiyekuwa Allaah. Lakini hata hivyo akasema kuwa kutafuta kinga sio ´ibaada na kwamba inajuzu. Unatakiwa kumwambia kuwa kutafuta ulinzi kwa Allaah ni ´ibaadah na kwamba kutafuta ulinzi kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah pekee ni shirki. Kwa kuwa mwenye kutafuta kinga kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika majanga ameshirikisha pamoja na Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye ndiye anayemjibu mwenye kudhikika anapomuomba na anaondoa madhara. Yeye ndiye Mwenye kuelekewa (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba kinga Kwake pale aliposema:

“Hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa isipokuwa Kwako.”[1]

قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ

“Sema: “Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah.”” (72:22)

وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ

“Naye ndiye Alindae na wala hakilindwi chochote kinyume Naye.” (23:88)

[1] al-Bukhaariy (5952), Muslim (2710), at-Tirmidhiy (3574), Abu Daawuud (5046), Ibn Maajah (3876), Ahmad (04/296) na ad-Daarimiy (2683).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 81
  • Imechapishwa: 08/01/2017