Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

86 – Hatuombi du´aa dhidi yao. Hatuondoi mkono katika kuwatii. Tunaona kuwa kuwatii wao ni kumtii Allaah (´Azza wa Jall) ambako amefaradhisha muda wa kuwa hawajaamrisha maasi. Tunawaombea kutengemaa na kusalimika.

MAELEZO

Hapana shaka kuwa Aayah inawahusu waislamu katika wao. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]

Kuhusu makafiri wa kikoloni, hawatakiwi kutiiwa. Bali ni wajibu kuwafanyia maandalizi kamili na kuisafisha miji kutokana na uchafu wao. Ama kufasiri maneno Yake (Ta´ala) ”katika nyinyi” (مِنكُمْ), kwamba ni ”kati yenu”, ni Bid´ah ya Qaadiyaaniyyah na upenyezaji wa kingereza ili kuwapotosha waislamu na kuwafanya wawatii makafiri wa kikoloni.

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 79
  • Imechapishwa: 08/10/2024