Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Katika kumuamini Allaah na Vitabu Vyake kunaingia kuamini ya kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah, imeteremshwa na si kiumbe. Uteremsho wake umeanza kutoka Kwake na Kwake itarudi. Allaah amezungumza kwayo maneno ya kihakika. Qur-aan hii iliyoteremshwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni maneno ya Allaah ya kihakika na sio maneno ya mwengine. Na wala haijuzu kusema ya kwamba ni masimulizi au ibara ya maneno ya Allaah, bali wanapoisoma watu au kuiandika ndani ya misahafu, kwa kufanya hivyo haijatoka kuwa maneno ya Allaah ya kihakika. Kwani mambo yalivyo ni kwamba maneno yananasibishwa kwa yule aliyeyatamka mwanzo, na si kwa yule aliyeyawakilisha na kuyafikisha. Hivyo ni maneno ya Allaah; herufi na maana yake. Maneno ya Allaah sio herufi bila ya maana na wala sio maana bila ya herufi.
MAELEZO
Katika kumuamini Allaah ni pamoja vilevile na kuamini kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Katika kuamini Vitabu vya Allaah ni pamoja na kuamini vilevile kwamba Qur-aan ni Kitabu kilichoteremshwa kwa mja na Mtume Wake ambaye ndiye Nabii wa mwisho, Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Qur-aan ni maneno ya Allaah, ni mamoja herufi na maana yake. Ni wajibu kuamini kuwa ni maneno ya Allaah na imeteremshwa na si kiumbe. Imeanza kutoka Kwake na Kwake itarudi. Pale inapoandikwa kwenye misahafu, inaposomwa na inapohifadhiwa haipingani na kuwa ni maneno ya Allaah. Imehifadhiwa kwenye vifua, imeandikwa kwenye misahafu na inasikiwa na masikio. Pamoja na haya yote bado ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall), ni mamoja herufi na maana yake. Haijuzu kusema kuwa Qur-aan ni masimulizi au ni ibara ya maneno ya Allaah, kama wanavyosema Ashaa´irah, Kullaabiyyah na wengineo. Qur-aan ni maneno ya Allaah herufi na maana yake na sio ibara wala masimulizi ya maneno ya Allaah. Ni maneno ya Allaah kwa dhati yake. Wakati Anaposema (Ta´ala):
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ
”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu.” (02:255)
ni maneno ya Allaah. Wakati Anaposema (Ta´ala):
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
“Sifa njema na shukurani zote ni za Allaah, Mola wa walimwengu.” (01:01)

وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا
”Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo.” (02:255)
ni maneno ya Allaah. Kila Aayah na kila neno yote hayo ni maneno ya Allaah, kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake, ni mamoja herufi na maana yake. Maneno ya Allaah sio harefi pasi na maana na wala sio maana pasi na herufi. Allaah amesema:

”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu.”
Haya ni maneno ya Allaah. Vivyo hivyo maana yake kuhusiana na uhai, kuyasimamia Kwake mambo, kuyalinda na kuyahifadhi Kwake mambo yote haya ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مِنَ الرَّحْمَـٰنِ
“Sema: “Nani [awezaye] kukulindeni usiku na mchana kutokana na [adhabu ya] Mwingi wa rehema?”” (21:42)
إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ
“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.” (35:10)
فَالْحُكْمُ لِلَّـهِ الْعَلِيِّ الْكَبِيرِ
“Basi leo hukumu ni ya Allaah pekee – Aliye juu, Mkubwa kabisa.” (40:12)
إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ
“Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, yukaribu.” (34:50)
إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Hakika Allaah ni Mwenye kusikia, Mjuzi.” (02:181)
وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Allaah ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.” (24:20)
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa yote haya, ni mamoja herufi na maana yake, ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 79-80
- Imechapishwa: 28/10/2024

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 79-80
Imechapishwa: 28/10/2024
https://firqatunnajia.com/53-yote-ndani-ya-qur-aan-ni-maneno-ya-allaah/