Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Katika hayo kunaingia vilevile kuamini ya kwamba Yuko karibu na ni Mwenye kuitikia. Amekusanya baina ya hayo katika maneno Yake:
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ
“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba; basi waniitikie Mimi na waniamini mimi wapate kuongoka.” (02:186)
Na maneo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia Maswahabah waliponyanyua sauti zao kwa Dhikr:
“Enyi watu! Zihurumieni nafsi zenu! Kwani hakika hamumuombi ambaye ni kiziwi wala asiyekuwepo. Hakika Yule mnayemwomba ni Mwenye kusikia Mwenye kuona na Aliye karibu. Hakika yule mnayemwomba Yuko karibu zaidi na mmoja wenu kuliko shingo ya vipando vyenu.”
Ukaribu na upamoja Wake yaliyotajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah hayapingani na yaliyotajwa ujuu Wake, kwani hakika Yeye (Subhaanah) hakuna kitu chochote mfano Wake katika sifa Zake zote. Naye Yuko juu kabisa kwa ukaribu Wake, karibu kwa utukufu Wake.
MAELEZO
Mtunzi (Rahimahu Allaah) amebainisha kuwa kunaingia katika kumuamini Allaah, majina na sifa Zake kuamini pia ya kwamba Yeye yukaribu na ni mwenye kuitikia (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye yuko juu ya ´Arshi. Hili halipingani na kuwa Kwake karibu na mwenye kuitikia (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye yuko juu kabisa kwa ukaribu Wake na yuko karibu kwa utukufu Wake, kama alivyosema mtunzi. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) yukaribu na ni mwenye kuitikia na wakati huohuo yuko juu (Subhaanahu wa Ta´ala). Yuko juu ya ´Arshi, juu ya mbingu zote na juu ya viumbe vyote. Kwa jili hii amesema (Ta´ala):

“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba; basi waniitikie Mimi na waniamini mimi wapate kuongoka.”
Hakika (Subhaanah) yuko karibu kwa mwenye kumuomba na ni Mwenye kuwaitikia waja Wake hekima Yake ikionelea kufanya hivyo.
Vilevile amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Pamoja na kuwa (Subhaabah) yuko juu ya ´Arshi halipingani na kuwa Kwake karibu, Mwenye kutikia na anasikia du´aa ya mwenye kumuomba. Yeye ndiye Mwenye kusikia du´aa, yuko karibu kwa kuitikia ni Mwenye kusikia na kuitikia (Subhaanahu wa Ta´ala). Amekariri hayo katika Aayah nyingi ambapo amejisifu ya kwamba ni Mwenye kusikia, anazisikia siri na minong´onezo na hakuna kinachojifichika Kwake (Jalla wa ´Alaa). Vivyo hivyo katika Hadiyth mbalimbali.
Yaliyotajwa kuhusu kuwepo Kwake juu hakupingani na kuwepo Kwake karibu na pamoja na viumbe. Yeye yuko pamoja na waja Wake kwa ujuzi Wake na kwa kuwaona:
هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاء وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
”Yeye ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anajua yanayoingia ardhini na yatokayo humo na yanayoteremka kutoka mbinguni na yanayopanda humo Naye yupamoja nanyi popote mlipo, na Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuyaona.” (57:04)
Vilevile yuko pamoja na mawalii Wake kwa ujuzi Wake, kuwahifadhi, kuwalinda, kuwanusuru na kuwatia nguvu (Subhaanahu wa Ta´ala).
Kwa hiyo ni wajibu kwa kila muumini mwanaume na mwanamke kuyaamini hayo na kwamba Yeye ni Mwenye kusikia na yuko karibu. Uwepo Wake (Jalla wa ´Alaa) juu ya ´Arshi haupingani kitu na kuwakaribia Kwake waja Wake na kuzisikia Kwake du´aa zao (Jalla wa ´Alaa). Yeye ni Mwenye kusikia na yukaribu, wakati huohuo yuko juu kabisa na ni Mkuu (Jalla wa ´Alaa). Amesema (Ta´ala):
وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ
”Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo – Naye ni yujuu kabisa, ametukuka kabisa.” (02:255)
إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ
“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.” (35:10)
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 77-79
- Imechapishwa: 28/10/2024

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 77-79
Imechapishwa: 28/10/2024
https://firqatunnajia.com/52-naye-yuko-juu-kabisa-kwa-ukaribu-wake-karibu-kwa-utukufu-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket