53. Ni ipi hukumu ya kuacha kuwaswalia Ahl-ul-Bid´ah?

Swali 53: Ni ipi hukumu ya kuacha kuwaswalia Ahl-ul-Bid´ah?

Jibu: Wanazuoni wakiacha kumswalia kwa lengo la kuwakimbiza watu kutokamana na matendo yao, ni jambo la sawa ikiwa Bid´ah zao hazipelekei katika kuwakufurisha. Ama ikiwa Bid´ah zao ni za kukufurisha, kama mfano wa Bid´ah za Khawaarij, Mu´tazilah na Jahmiyyah, haifai kuwaswalia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 40
  • Imechapishwa: 25/12/2021