53. Ndio maana pengine mipango ya biashara yako isifaulu

50 – Ibn Mas´uud amesema:

”Wakati mja anapofikiria kufanya jambo la kibiashara au la kiutawala, ambapo jambo likamkuwia jepesi, Allaah akamtazama kutokea juu ya mbingu ya saba na akawaambia Malaika: ”Liondosheni kwake! Kwa sababu nikimfanyia nalo wepesi, basi nitamwingiza kwa ajili yake Motoni.”[1]

 Ameipokea al-Laalakaa´iy kwa cheni ya wapokezi yenye nguvu[2].

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim katika “Ijitimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”. ad-Daarimiy  amepokea mfano wake katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 26.

[2] Ameipokea al-Laalakaa´iy katika “Sharh Usuwli I´tiqaadi Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” kwa cheni ya wapokezi dhaifu, kama alivyoashiria hivo mtunzi, kupitia kwake ameipokea mtunzi wa kitabu.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 104
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy