1 – Mke mbaya ni ugonjwa usiyoponeka. Kumuoa mwanamke mtumzima kunaondosha haya. Kuwatii wanawake kunawatweza wenye busara.
2 – Waigilize wenye busara, utakuwa mmoja wao. Jipinde juu ya utukufu, utaufikia.
3 – Mtu hutambulika kupitia rafiki yake. Tahadhari kutokamana na marafiki waovu. Humsaliti na kumsononesha rafiki. Ukaribu nao unaambukiza zaidi kuliko upele. Kujitenga mbali nao ni katika adabu.
4 – Kuna marafiki sampuli mbili. Wa kwanza anakuhifadhi wakati wa matatizo. Mwingine ni yule ambaye ni rafiki yako kipindi cha raha peke yake. Mlinde rafiki wa kipindi cha matatizo na mwepuke rafiki wa ustawi. Wao ni maadui waovu mno.
5 – Jiweke mbali na kueneza ufisadi ardhini ijapo utakuwa katika nchi ya maadui. Usiishushe heshima yako kwa ambaye yuko chini yako.
6 – Tahadhari na kuangaza sana na kuwa mlaini sana. Mtu kama huyo hunasibishwa na mambo ya kike. Jiepushe na kuwazungumzisha wanawake maneno ya kimapenzi na ya ladha.
7 – Mjinga kukusema vibaya ni bora kuliko yeye kukusifu. Kuitambua haki ni katika sifa za wakweli.
8 – Yule mwenye kuhitaji anadharauliwa. Hana mengi ya kusema na anaogopa kukataliwa.
9 – Ifanye Siwaak kuwa ni katika maumbile yako. Wakati unapoitumia basi piga kandokando.
10 – Yule anayeitukuza heshima yake hutukuzwa na watu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 201-202
- Imechapishwa: 21/08/2021
1 – Mke mbaya ni ugonjwa usiyoponeka. Kumuoa mwanamke mtumzima kunaondosha haya. Kuwatii wanawake kunawatweza wenye busara.
2 – Waigilize wenye busara, utakuwa mmoja wao. Jipinde juu ya utukufu, utaufikia.
3 – Mtu hutambulika kupitia rafiki yake. Tahadhari kutokamana na marafiki waovu. Humsaliti na kumsononesha rafiki. Ukaribu nao unaambukiza zaidi kuliko upele. Kujitenga mbali nao ni katika adabu.
4 – Kuna marafiki sampuli mbili. Wa kwanza anakuhifadhi wakati wa matatizo. Mwingine ni yule ambaye ni rafiki yako kipindi cha raha peke yake. Mlinde rafiki wa kipindi cha matatizo na mwepuke rafiki wa ustawi. Wao ni maadui waovu mno.
5 – Jiweke mbali na kueneza ufisadi ardhini ijapo utakuwa katika nchi ya maadui. Usiishushe heshima yako kwa ambaye yuko chini yako.
6 – Tahadhari na kuangaza sana na kuwa mlaini sana. Mtu kama huyo hunasibishwa na mambo ya kike. Jiepushe na kuwazungumzisha wanawake maneno ya kimapenzi na ya ladha.
7 – Mjinga kukusema vibaya ni bora kuliko yeye kukusifu. Kuitambua haki ni katika sifa za wakweli.
8 – Yule mwenye kuhitaji anadharauliwa. Hana mengi ya kusema na anaogopa kukataliwa.
9 – Ifanye Siwaak kuwa ni katika maumbile yako. Wakati unapoitumia basi piga kandokando.
10 – Yule anayeitukuza heshima yake hutukuzwa na watu.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 201-202
Imechapishwa: 21/08/2021
https://firqatunnajia.com/53-nasaha-za-al-khattwaab-al-makhzuumiy-al-qurashiy-kwa-mwanae-iv/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)