Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
”Ana haki tu ya kujitetea mahala hapo. Anuie kutomuua yeyote. Ikitokea wakati wa kuitetea nafsi yake akamuua yule mshambulizi, basi atajaza yule mshambulizi.”
Hapa kunabainishwa namna anavyotakiwa kujitetea dhidi ya yule mshambuliaji. Anatakiwa kujitetea vipi yeye na mali yake dhidi ya waasi, wezi na majambazi? Kujitetea inatakiwa iwe kwa kile kiwango tu ambacho kinahitajika ili kuzuia tishio. Ikiwa yule mshambuliaji anataka kumuua yule anayemsahmbulia, kupora mali yake au kuvunja heshima yake, basi inafaa kwake kujitetea ijapo ni kwa kumuua. Yule mshamuliwaji anapaswa kuwa na nia njema na asinuie kumuua yeyote – yeye anachotaka ni kuzuia khatari inayomwelekea. Hata hivyo hapana vibaya na hapati dhambi ikipelekea kuuliwa kwa yule mshamuliaji. Akiuliwa wakati akijaribu kuitetea nafsi yake, mali yake na heshima yake anazingatiwa amekufa shahidi. Hayo ni kutokana na Hadiyth kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:
“Kuna mtu alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unaonaje iwapo atakuja mtu anayetaka kuchukua mali yangu?” Akasema: “Usimpe.” Akauliza: “Akinipiga vita?” Akajibu: “Mpige vita.” Akauliza: “Akiniua?” Akajibu: “Basi wewe utakuwa shahidi.” Akauliza: “Nikimuua?” Akajibu: “Basi yeye ataingia Motoni.”[1]
Kwa hivyo anakufa hali ya kuwa ni shahidi kwa sharti awe ni muumini. Yule mshambuliaji amejisababishia mwenyewe maangamivu, khaswa ikiwa kama atauliwa. Katika hali hiyo Allaah amemuharakishia adhabu yake duniani na huko Aakhirah ndiye atakayemua la kumfanya.
[1] Muslim (140).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 131-132
- Imechapishwa: 19/05/2026
Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
”Ana haki tu ya kujitetea mahala hapo. Anuie kutomuua yeyote. Ikitokea wakati wa kuitetea nafsi yake akamuua yule mshambulizi, basi atajaza yule mshambulizi.”
Hapa kunabainishwa namna anavyotakiwa kujitetea dhidi ya yule mshambuliaji. Anatakiwa kujitetea vipi yeye na mali yake dhidi ya waasi, wezi na majambazi? Kujitetea inatakiwa iwe kwa kile kiwango tu ambacho kinahitajika ili kuzuia tishio. Ikiwa yule mshambuliaji anataka kumuua yule anayemsahmbulia, kupora mali yake au kuvunja heshima yake, basi inafaa kwake kujitetea ijapo ni kwa kumuua. Yule mshamuliwaji anapaswa kuwa na nia njema na asinuie kumuua yeyote – yeye anachotaka ni kuzuia khatari inayomwelekea. Hata hivyo hapana vibaya na hapati dhambi ikipelekea kuuliwa kwa yule mshamuliaji. Akiuliwa wakati akijaribu kuitetea nafsi yake, mali yake na heshima yake anazingatiwa amekufa shahidi. Hayo ni kutokana na Hadiyth kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:
“Kuna mtu alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unaonaje iwapo atakuja mtu anayetaka kuchukua mali yangu?” Akasema: “Usimpe.” Akauliza: “Akinipiga vita?” Akajibu: “Mpige vita.” Akauliza: “Akiniua?” Akajibu: “Basi wewe utakuwa shahidi.” Akauliza: “Nikimuua?” Akajibu: “Basi yeye ataingia Motoni.”[1]
Kwa hivyo anakufa hali ya kuwa ni shahidi kwa sharti awe ni muumini. Yule mshambuliaji amejisababishia mwenyewe maangamivu, khaswa ikiwa kama atauliwa. Katika hali hiyo Allaah amemuharakishia adhabu yake duniani na huko Aakhirah ndiye atakayemua la kumfanya.
[1] Muslim (140).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 131-132
Imechapishwa: 19/05/2026
https://firqatunnajia.com/53-lengo-la-kujitetea/