Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
Inafaa kuwapiga vita wezi na Khawaarij. Wakimshambulia mtu au mali yake basi inafaa kwake kupambana kwa ajili ya nafsi yake na mali yake. Ajitetee kwa yote ayawezayo. Hata hivyo haifai kwake kuwafuata au kuwatafuta wakimuacha. Hakuna mwingine isipokuwa kiongozi au mtawala wa waislamu ndiye anayeweza kufanya kitu kama hicho. Ana haki tu ya kujitetea mahala hapo. Anuie kutomuua yeyote. Ikitokea wakati wa kuitetea nafsi yake akamuua yule mshambulizi, basi atajaza yule mshambulizi.
MAELEZO
Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya waasi na majambazi. Wakiwavamilia waislamu au wakamfanyia uasi kiongozi anayekubalika kwa mujibu wa Shari´ah au wao kwa wao, inafaa kuwapiga vita kutokana na maneno Yake Allaah (Ta´ala):
فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
“… lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee katika amri ya Allaah. Likishaelemea, basi suluhisheni kati yao kwa uadilifu na tendeni haki. Kwani hakika Allaah anawapenda wanaotenda haki. Hakika mambo yalivyo ni kwamba waumini ni ndugu, hivyo basi suluhisheni kati ya ndugu zenu na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa.”[1]
Kundi dhalimu linatakiwa kupiwa vita ni mamoja linamshambulia mtawala au wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kama yapo mamlaka basi ndio yanayotakiwa kuingilia suala hili ili kusimwagike damu kati ya makundi hayo mawili. Kama hakuna mamlaka basi lile kundi lililovamiliwa linayo haki ya kujitetea yeye, mali yake na heshima zao ijapo ni kwa kuwaua wale washambulizi, kwa sababu wao wenyewe wanachotaka ni kumwaga damu, kupora mali na kuvunja heshima. Kujitetea inatakiwa iwe kwa kile kiwango tu ambacho kinahitajika ili kuzuia tishio. Inafaa kwa yule aliyevamiwa kujitetea dhidi ya waasi na majambazi. Aidha ni lazima kwa waislamu wengine kuwasaidia na kuwanusuru wale wanaoshambulia kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ
“… lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee katika amri ya Allaah… ”
Bi maana mpaka lile kundi lenye kushambulia lirejee katika haki. Pindi wataporejea katika haki hawatolipizwa kisasi baada ya hapo. Na wakikimbia kutoka katika uwanja wa vita haitakiwi kuwafuatilia, kuwaua wala kuwapora. Kwa sababu kilicho muhimu ni kule kufaa kuwapiga vita mpaka warejee kwenye haki na kuacha hali yao mbaya. Kisha baada ya hapo wasitishiwe maisha tena. Hii ndio hukumu ya waasi, wezi na majambazi. Kama kuna mamlaka ya Kishari´ah itasimamisha juu yao Shari´ah ya Allaah. Kama hakuna kiongozi, basi kila anayeshambuliwa anayo haki ya kujitetea yeye, mali yake na heshima yake ijapo ni kwa kumuua yule mshambulizi. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya suala hili.
[1] 49:9-10
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 130-131
- Imechapishwa: 19/05/2026

Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 130-131
Imechapishwa: 19/05/2026
https://firqatunnajia.com/52-kujitetea-dhidi-ya-khawaarij-na-majambazi/