Swali 52: Tumswalie tukijua kuwa maiti ni mnafiki[1]?

Jibu: Haswaliwi. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا

“Wala usimswalie yeyote kabisa miongoni mwao akifa.[2]

Hapa ni pale ambapo ikiwa unafiki wake ni wa dhahiri. Ama ikiwa inahusiana na tuhuma peke yake, anaswaliwa. Kwa sababu kimsingi ni ulazima wa kumswalia maiti muislamu. Hivyo wajibu hauachwi kwa sababu ya kuwa shaka.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/160).

[2] 9:84

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 24/12/2021