52. Du´aa ya kufungulia swalah inasomwa katika kila Rak´ah kwenye Tarawiyh?

Swali: Je, du´aa ya kufungulia swalah inasomwa katika kila Rak´ah ya Tarawiyh? Kipi unachowanasihi wale maimamu wanaotosheka kusoma Tashahhud ya kwanza peke yake katika Tarawiyh?

Jibu: Tarawiyh inazingatiwa kuwa swalah moja. Tukiianza swalah kwa du´aa ya kufungulia swalah baada ya Takbiyr, basi tunatosheka nayo katika Rak´ah zilizobaki. Ni kama ambavo sisi katika swalah ya faradhi tunatosheka na du´aa ya kufungulia swalah inayosomwa katika ile Rak´ah ya kwanza.

Imewekwa katika Shari´ah kwa imamu kukamilisha Tashahhud ya mwisho. Kuomba du´aa ndani ya swalah ndio bora kuliko kuomba du´aa nje yake, kwa sababu ndani ya swalah tuko katika ´ibaadah na utiifu. Kwa ajili hiyo hatutakiwi kufanya haraka sana kiasi cha kwamba tukaacha yale mambo mengi yaliyopendekezwa. Bali tunatakiwa tuswali kwa utaratibu na tukakamilishe yale mambo yaliyopendekezwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 07/04/2022