´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kila kitu kina kisafishaji na hakika kisafishaji cha nyoyo ni kumtaja Allaah (‘Azza wa Jall). Hakuna kitu chochote kinachookoa zaidi kutokana na adhabu ya Allaah kama kumtaja Allaah (‘Azza wa Jall).” Wakasema: ”Hata jihaad katika njia ya Allaah (‘Azza wa Jall)?” Akasema: ”Hata kama atapigana kwa upanga wake mpaka ukavunjika.”[1]
Ameipokea al-Bayhaqiy.
Hapana shaka kuwa moyo hujaa kutu kama vile shaba na fedha vinavyojaa kutu. Kisafishaji chake ni Dhikr. Hakika Dhikr humsafisha mpaka uwe kama kioo cheupe. Basi anapokiacha moyo unajaa kutu, na anapokitakasa kinakuwa safi.
Kutu ya moyo ni kwa mambo mawili: kwa kughaflika na kwa dhambi. Kisafishaji chake ni kwa mambo mawili: kwa kuomba msamaha na kwa Dhikr. Yeyote ambaye kughafilika ndio kumetawala muda wake mwingi, basi kutu huwa imejaa juu ya moyo wake na kutu hiyo huwa kwa kiasi cha kughafilika kwake. Moyo unapojawa na kutu, basi hauwezi kuchukua picha ya mambo yaliyojulikana jinsi yalivyo. Hivyo huona batili kwa sura ya haki na haki huiona kwa sura ya batili. Kwa sababu kutu inapojilimbikiza juu yake, huufanya kuwa na giza na hivyo picha ya ukweli hazionekani jinsi zilivyo.
Ikiwa kutu itarundikana na kuwa nyeusi na likamshukia giza linalofunika moyo, basi uwezo wake wa kutambua na kuelewa unaharibika. Matokeo yake hapokei haki wala hakemei batili. Hii ni miongoni mwa adhabu kubwa zaidi ya moyo. Chanzo cha hayo ni kughafilika na kufuata matamanio. Hakika viwili hivyo huzima nuru ya moyo na hupofusha macho yake. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا
“Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake kutokana na ukumbusho Wetu akafuata matamanio yake na jambo lake likawa lenye kuzidi kuvuka mipaka.”[2]
Kwa hiyo mja anapotaka kumuiga mtu mwingine, basi atazame kama ni miongoni mwa watu wa wanaomtaja Allaah au ni katika waghafilikaji. Je, kinachomtawala ni matamanio au wahy? Kama ni miongoni mwa watu wanaotawaliwa na matamanio na walioghafilika, basi mambo yake yameparanganyika. Hivyo asimuige, kwa sababu atamwangamiza.
Kuvuka mipaka kumefasiriwa kuangamia. Kwa msemo mwingine ni kuwa huyo amepotoka na akapuuza amri ambayo inamlazimu kuifuata na kuifanyia kazi na ambayo ndio yenye mwongozo na mafanikio yake. Pia imefasiriwa kama israfu. Tafsiri ya tatu ni maangamizo. Vilevile imefasiriwa kwenda kinyume na haki. Zote hizi zimekaribiana. Makusudio ni kwamba Allaah (Ta´ala) amekataza kumtii ambaye amekusanya sifa hizi. Ni wajibu kwa mtu kumchunguza mwalimu wake, kiongozi wake au anayemwiga. Kama atamkuta hivyo, basi na ajitenge naye. Na akimuona ni miongoni mwa waliotawaliwa na kumtaja Allaah (Ta´ala), wakafuata Sunnah na jambo lake halijaparanganya, bali ni mwenye msimamo mkali juu ya nafsi yake katika amri ya Allaah, basi ashikamane naye barabara.
Hapana tofauti baina ya aliye hai na aliyekufa isipokuwa kwa Dhikr. Basi mfano wa anayemtaja Mola wake na asiyemtaja Mola wake ni kama mfano wa aliye hai na aliyekufa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mtajeni Allaah (Ta´ala) kwa wingi mpaka kusemwe mwendawazimu.”[3]
[1] Shu´b-ul-Iymaan (2/418-419). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (1932).
[2] 18:28
[3] Ahmad (4/173), Ibn Hibbaan (817), ambaye ameisahihisha, na al-Haakim (1/499), ambaye amesahihisha cheni ya wapokezi wake na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (1108).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 91-93
- Imechapishwa: 18/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 91-93
Imechapishwa: 18/08/2025
https://firqatunnajia.com/51-moyo-uliyopatwa-na-kutu/